Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 21:34

Serikali ya waziri mkuu wa Israel Netanyahu yapiga kura kufunga ofisi za Al Jazeera

Mtu aonekana akibeba vifaa vya vyombo vya habari kufuatia uvamizi wa polisi wa Israel kwenye ofisi ya Al Jazeera katika hoteli ya Ambassador mjini Jerusalem, Mei 5, 2024. Picha ya Reuters.
Mtu aonekana akibeba vifaa vya vyombo vya habari kufuatia uvamizi wa polisi wa Israel kwenye ofisi ya Al Jazeera katika hoteli ya Ambassador mjini Jerusalem, Mei 5, 2024. Picha ya Reuters.

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu Jumapili amesema kwamba serikali yake imepiga kura kwa kauli moja kufunga ofisi za kituo cha matangazo cha Al-Jazeera kinachomilikiwa na Qatar.

Netanyahu alitangaza uamuzi huo kwenye mtandao wa X, lakini maelezo kuhusu athari za hatua hiyo kwa kituo hicho, lini itaanza kutekelezwa au ikiwa hatua hiyo ni ya kudumu au ya muda hayakutolewa wazi mara moja.

Mwandishi wa Al Jazeera katika idhaa ya Kiarabu amesema uamuzi huo utaathiri matangazo yake nchini Israel na Jerusalem mashariki, ambako kituo hicho kimekuwa kikiperusha matangazo ya moja kwa moja kwa miezi kadhaa tangu shambulio la Oktoba 7 ambalo lilichochea vita huko Gaza.

Forum

XS
SM
MD
LG