Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 04:10

Ruto atoa wito wa mabadiliko ya taasisi za kifedha


Rais wa Kenya William Ruto wakati wa mkutano wa pamoja wa vyombo vya habari na Rais wa Marekani huko White House Mei 23, 2024.. Picha na REUTERS/Nathan Howard
Rais wa Kenya William Ruto wakati wa mkutano wa pamoja wa vyombo vya habari na Rais wa Marekani huko White House Mei 23, 2024.. Picha na REUTERS/Nathan Howard

Rais William Ruto wa Kenya amesema kuwa ni muhimu kufanya mfumo fedha wa kimataifa uwe mwepesi zaidi ili kuzisaidia nchi kupambana na majanga, na karibisha uungaji mkono wa Marekani wa kufanya mageuzi kama hayo.

Akizungumza Alhamisi wakati wa kuanza mkutano wa pamoja na mwenyeji wake Rais wa Marekani Joe Biden, Ruto amesema hivi karibuni aliitisha mkutano wa kilele kwa Idara ya Maendeleo ya Kimataifa ya Benki ya Dunia kuzungumzia suala la madeni ya mataifa mengi yenye kipato cha chini.

Amesema lengo lilikuwa kutafuta njia za kufanya taasisi za fedha kuwa “nyeti, haraka na kuweza kujibu matatizo yanayochangiwa na mabadiliko ya hali ya hewa, mfumko wa bei na viwangi vya riba.”

Viongozi wa Afrika mwezi uliopita waliitisha mkutano na nchi tajiri kuahidi kutoa mchango mkubwa ambao haujawahi kutolewa wa karibu dola bilioni 120 kwenye idara hiyo, uwepo kwa kiwango kidogo cha riba ambacho nchi zinazoendelea kinategemea kusaidia kugharimia maendeleo yao na kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa.

Wafadhili watatoa ahadi za fedha taslimu kwa idara hiyo ambayo itatoa mikopo ya muda mrefu wenye riba ya kiwango cha chini, wakati wa mkutano utakaofanyika Japan mwezi Desemba.

Marekani na nchi nyingine zimeweka shinikizo za mabadiliko katika Benki ya Dunia na mabenki mengine ya maendeleo kuongeza uwezo wao wa kukopesha ili kuweza kuzisaidia vyema nchi zenye kipato cha chini kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa na kuzoea mazingira ya kazi ya kijitali zaidi.

Biden na Ruto wanazindua mpango unaoitwa Nairobi-Washington Vision ili kuihimiza jumuiya ya kitaifa kuunga mkono zaidi nchi ambazo zinataka kufanya mageuzi na kuwekeza katika maendeleo yao lakini zinashindwa kutokana na mzigo mzito wa madeni.

Forum

XS
SM
MD
LG