Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 06, 2024 Local time: 02:25

Marekani kuitambua Kenya kama mshirika wake wa kwanza asiyekuwa mwanachama wa NATO


Mke wa Rais wa Marekani Jill Biden akisalimiana na Rais wa Kenya William Ruto na mkewe, Rachel Ruto walipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Andrews katika jimbo la Maryland, Mei 22, 2024. Picha ya AFP
Mke wa Rais wa Marekani Jill Biden akisalimiana na Rais wa Kenya William Ruto na mkewe, Rachel Ruto walipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Andrews katika jimbo la Maryland, Mei 22, 2024. Picha ya AFP

Marekani itaitambua Kenya kama mshirika wake wa kwanza asiyekuwa mwanachama wa NATO katika eneo la kusini mwa Jangwa la Sahara, White House imesema wakati Rais Joe Biden alipomkaribisha Rais William Ruto katika ziara ya kiserikali.

Kutambuliwa huko kunazipa nchi ambazo sio wanachama wa muungano wa NATO kunufaika na misaada ya kijeshi na fedha kama nchi wanachama wa NATO, lakini bila makubaliano ya pande zote kuhusu ulinzi ambayo yanaunganisha nchi wanachama wa NATO.

Afisa mkuu wa utawala wa Biden aliwaambia waandishi wa habari Jumatano kwamba Biden atalitaarifu Bunge la Marekani kuhusu utambuzi huo, ambako unachukua siku 30 kabla ya kuanza kutekelezwa.

Afisa huyo alisema hatua hiyo inalenga kuiinua Kenya na kukiri kweli kwamba Kenya ni mshirika wa Marekani kimataifa.

Wakati huo huo, Ruto na Biden watatumia majadiliano yao ya leo kutafuta suluhu ya mpango wa Kenya wa kutuma maafisa wa polisi 1,000 nchini Haiti.

Mpango huo ambao Marekani imeahidi kutoa ufadhili wa dola milioni 300, unakabiliwa na changamoto kubwa za kisiasa na kisheria nchini Kenya.

Forum

XS
SM
MD
LG