Mokhber mwenye umri wa miaka 68, kwa kiasi kikubwa alikuwa haonekani sana hadharani ikilinganishwa na wanasiasa wengine katika utawala wa Iran.
Baada ya kifo cha Raisi kwa kumjibu wa katiba kimemweka Mokhber hadharani. Anatarajiwa kuhudumu kama rais wa mpito kwa siku 50 kabla ya uchaguzi wa lazima wa rais nchini Iran.
Kiongozi mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei alitangaza kuteuliwa kwa Mokhber katika ujumbe wa salamu za rambirambi kufuatia kifo cha Rais katika ajali ya helikopta Jumapili. Helikpota hiyo ilipatikana Jumatatu kaskazini magharibi mwa nchi.
Licha ya kutokuwa na hadhi kubwa kwa umma, Mokhber alishikilia nyadhifa muhimu ndani ya muundo wa utawala wa nchi, hasa katika mashirika ya hisani. Mashirika hayo yaliundwa kwa wingi kutokana na michango ya fedha au mali zilizokamatwa baada ya mapinduzi ya Iran ya 1979.
Forum