Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 23:44

Wabunge wa EU waidhinisha sheria ya uhamiaji


Bunge la Umoja wa Ulaya.
Bunge la Umoja wa Ulaya.

Wabunge wa Umoja wa Ulaya Jumatano wameidhinisha sheria ya uhamiaji, kwa matumaini ya kumaliza miaka kadhaa ya migawanyiko juu ya jinsi ya kushughulikia kuingia kwa maelfu ya watu katika bara hilo bila ya idhini.

Hatua hiyo imeinyima ushindi kampeni ya mrengo wa kulia kuhusu suala hilo kabla ya uchaguzi wa mwezi Juni.

Katika mfululizo wa kura 10, wanachama wa bunge la Ulaya wameidhinisha kanuni na sera ambazo zinahusu mkataba wa Uhamiaji na Hifadhi.

Mageuzi yanazungumzia suala zito la nani ana wajibu kwa wahamiaji wakati wanapowasili na iwapo nchi nyingine za EU ni vyema ziwajibike katika kusaidia.

Nchi wanachama 27 wa EU lazima hivi sasa waidhinishe mpango wa mageuzi, kuna uwezekano kura itapigwa mwishoni mwa mwezi huu, kabla ya sheria kuazna kufanya kazi.

Roberta Metsola
Roberta Metsola

Rais wa bunge la Ulaya, Roberta Metsola, ambaye alikuwa mbunge wa juu katika suala la uhamiaji ambaye alisaida kufungua njia kwa mpango wa mageuzi, amesema EU hivi sasa ina mfumo thabiti wa kisheria ambao “utalinda mipaka ya Ulaya.”

Forum

XS
SM
MD
LG