Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Novemba 24, 2024 Local time: 01:47

Umoja wa Ulaya umetangaza msaada wa dola bilioni nane kwa Misri


Rais wa Tume ya Ulaya, Ursula von der Leyen akiwa mjini Brussels. February 21, 2024.
Rais wa Tume ya Ulaya, Ursula von der Leyen akiwa mjini Brussels. February 21, 2024.

Makubaliano hayo yamepangwa kutiwa saini wakati wa ziara ya rais wa Tume ya Ulaya, Ursula von der Leyen

Umoja wa Ulaya umetangaza msaada wa dola bilioni 8 kwa ajili ya Misri iliyokumbwa na uhaba wa fedha huku kukiwa na wasiwasi kwamba shinikizo la kiuchumi na mizozo na machafuko katika nchi jirani huenda vikawasukuma wahamiaji wengi zaidi katika fukwe za Ulaya.

Makubaliano hayo yamepangwa kutiwa saini wakati wa ziara ya rais wa Tume ya Ulaya, Ursula von der Leyen na viongozi wa Ubelgiji, Italia, Austria, Cyprus na Ugiriki, kulingana na maafisa wa Misri.

Msaada huo unajumuisha misaada na mikopo katika kipindi cha miaka mitatu ijayo kwa nchi hiyo yenye idadi kubwa ya watu katika ulimwengu wa Kiarabu, kwa mujibu wa ujumbe wa Umoja wa Ulaya mjini Cairo.

Kulingana na hati kutoka kwa ujumbe wa EU nchini Misri, pande hizo mbili zimekuza ushirikiano wao kwa kiwango cha “ushirikiano wa kimkakati na wa kina”, na kufungua njia ya kupanua ushirikiano wa Misri na EU katika maeneo mbalimbali ya uchumi na yasiyo ya uchumi.

Forum

XS
SM
MD
LG