Haikufamika wazi mara moja nani alihusika na mashambulizi hayo ya anga katika mkoa wa mashariki mwa Syria wa Deir el-Zour ambao unapakana na Iraq.
Shirika linalofuatilia haki za binadamu lenye makao yake Uingereza, lilisema mashambulizi hayo yaliua watu 15, akiwemo mshauri wa kikosi cha mapinduzi cha Iran, walinzi wake wawili, pamoja na wapiganaji tisa wa Iraq wa kundi linaloungwa mkono na Iran na raia wawili wa Syria wanaofanya kazi na Wairan.
Limeongeza kuwa muhandisi raia wa Syria aliuawa pia.
Shirika la habari la serikali ya Iran limethibitisha kwamba mwanachama wa kikosi cha mapinduzi aliuawa nchini Syria.
WHO imesema mmoja wa wafanyakazi wake, muhandisi Emad Shebab aliuawa katika moja ya mashambulizi dhidi ya jengo lake.
Forum