Ujerumani wiki iliyopita iliwatuhumu majasusi wa kijeshi wa Russia kwa udukuzi kwenye akaunti za viongozi wa juu wa chama cha Social Democrats cha Scholz na malengo mengine kadhaa nyeti ya serikali na viwanda.
Berlin imeungana na NATO na nchi za Ulaya katika kutahadharisha kuwa ujasusi wa mitandaoni wa Russia utakuwa na madhara.
Ofisi ya Mambo ya Nje mjini Berlin ilisema Jumatatu kuwa serikali inalichukulia tukio la hivi karibuni “kwa uzito mkubwa” na kuwa Waziri wa Mambo ya Nje Annalena Baerbock aliamua kumrejesha nyumbani Balozi wa Ujerumani Alexander Lambsdorff, atarejea Moscow baada ya wiki moja.
“Serikali ya Ujerumani inalichukulia tukio hili kwa umuhimu mkubwa kwani vitendo hivi dhidi ya demokrasia huru na taasisi zake zinazoiunga mkono,” msemaji wa ofisi ya mambo ya nje Kathrin Deschauer alisema.
Forum