Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 07:57

Viongozi wa EU wakutana Paris kujadili kuhusu misaada ya kibinadamu kwa Sudan


Mwakilishi wa EU kwenye masuala ya Kigeni na sera za Usalama Josep Borrell, mmoja wanadiplomasia wanaokutana Paris.
Mwakilishi wa EU kwenye masuala ya Kigeni na sera za Usalama Josep Borrell, mmoja wanadiplomasia wanaokutana Paris.

Waziri wa mambo ya nje  wa Ujerumani Annalena Baerbock amesema  Jumatatu kwamba taifa lake litatoa msaada wa kibinadamu  wa euro milioni 244 zaidi kwa Sudan, taifa lililokumbwa na vita.

Hayo amesema wakati wanadiplomasia wa Ulaya walipokutana mjini Paris Ufaransa ikiwa mwaka mmoja tangu kuzuka kwa ghasia nchini Sudan. “Kwa pamoja tunaweza kuzuia baa la njaa, lakini hilo litategemea ushirikiano wetu."

Baerbock amesema kuwa huenda watu milioni moja wataangamia kutokana na njaa nchini humo mwaka huu, iwapo hatua za dharura hazitachukuliwa.Marekani ambayo inatarajia kuwa kikao hicho cha Paris kitashawishi misaada zaidi kutoka mataifa mengine pia inapanga kutangaza nyongeza ya msaada wa dola milioni 100 kwa taifa hilo.

Miongoni mwa wanadiplomasia wengine kwenye kikao hicho ni pamoja na waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa Stephane Sajourn na mwanadipomasia wa juu wa EU Josep Borrell, pamoja na kamishna wa kuratibu majanga wa EU. Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amepangiwa kukutana na Borrell, pamoja na wenzake mwishoni mwa kikao hicho, ofisi ya masuala ya nje ya EU imesema.

Forum

XS
SM
MD
LG