Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 14:02

Polisi wa Uhispania wakamata genge la utepeli katika biashara ya bangi


Polisi wakiongozwa na Uhispania wamekamata genge ambalo linadaiwa kulaghai dola milioni zaidi ya 686 kutoka kwa watu katika nchi 35 katika udanganyifu unaohusu bangi kwa ajili ya matumizi ya kitabibu.

Genge hilo liliweka mfumo wa uuzaji na kuhudhuria maonyesho ya kimataifa ya bangi na kushawishi waathiriwa kuwekeza katika mfumo huo, polisi wa kitaifa wa Uhispania wamesema katika taarifa.

Polisi wa Uhispania waliongoza operesheni hiyo kwa msaada wa polisi wa Ulaya, Europol na mataifa mengine matano.

Washukiwa tisa ambao hawajatajwa majina walizuiliwa Aprili 11 kwa tuhuma za ulaghai katika nchi za Uhispania, Uingereza, Ujerumani, Latvia, Poland, Italia na Jamhuri ya Dominika.

Silvia Garrido msemaji wa polisi wa Uhispania amesema mtindo wa biashara uliotolewa na shirika hilo ulihusisha kutumia mtaji uliohamishwa kutoka kwa wawekezaji ili kuendeleza ushirikiano wa kilimo cha bangi.

Forum

XS
SM
MD
LG