Hata hivyo Blinken amesema hatua hizo hazitoshi kukidhi matakwa ya utawala wa Rais Joe Biden kwa ajili ya kuboresha hali ya kibinadamu katika eneo hilo.
Waziri Blinken amefafanua Ijumaa kwamba mpaka pale hatua hizo zitakapo tekelezwa kikamilifu, kufunguliwa vivuko zaidi vya mpakani kunaweza kuongeza misaada kwa Wapalestina waliojikuta katika mapigano baina ya Israel na Hamas.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani ameeleza haya:
“ Haya ni maendeleo chanya, lakini mtihani wa kweli ni matokeo na ndiyo tunacho tazamia kuona katika siku za karibuni na wiki zijazo. Je misaada inawafikia watu wenye shida, kote Gaza?
Je ucheleweshwo mwingine kwenye vivuko vya mpakani umetatuliwa? Je tuna mfumo bora zaidi wa kutatua mgogoro na uratibu ili wafanyakazi wa misaada, wanaopeleka msaada wanaweza kufanya hivyo kwa hali salama na yenye uhakika? Mambo yote haya ni muhimu , na yana hitaji kupimwa na matokeo.”
Ofisi ya waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ilitangaza Ijumaa kwamba Israel itachukua hatua kuboresha hali ikiwemo kufungua kivuko muhimu cha mpaka kuingia Gaza saa kadhaa baada ya rais wa Marekani Joe Biden kumwambia Alhamisi kwa njia ya simu kwamba msaada wa Marekani kwa ajili ya vita huko Gaza utategemea na Israel kuchukua hatua zaidi kuwalinda raia na wafanyakazi wa msaada.
Forum