Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 04:20

Rais Biden na Netanyahu wanafanya mazungumzo ya simu kuhusu Gaza


Rais Joe Biden wa Marekani (L) na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu
Rais Joe Biden wa Marekani (L) na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Marekani anasema Israel inahitaji hatua bora kuwalinda wafanyakazi wa misaada ya kibinadamu na raia.

Wito zaidi umetolewa Alhamisi kwa Israel kuhusika kwake na shambulizi lake la anga dhidi ya msafara huko Gaza uliowaua wafanyakazi saba wa misaada kutoka kundi la World Central Kitchen.

Rais wa Marekani Joe Biden na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu wanatarajiwa kuzungumza kwa simu leo Alhamisi ikiwa ni ya kwanza tangu shambulio hilo.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani Matthew Miller amewaambia waandishi wa habari Jumatano kuwa Israel inahitaji hatua bora zaidi kuwalinda wafanyakazi wa misaada ya kibinadamu na raia.

Kundi la World Central Kitchen limesema kuwa limezitaka Australia, Uingereza, Canada, Poland na Marekani kudai uchunguzi huru, na wa tatu kuhusu mashambulizi hayo, ikijumuisha kama yalifanywa kwa makusudi au vinginevyo yalikiuka sheria za kimataifa.

Forum

XS
SM
MD
LG