Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Novemba 24, 2024 Local time: 01:36

Israel yasema inachukua hatua kuwezesha ufikishaji wa misaada ya kibinadamu katika Ukanda wa Gaza


Gari la kijeshi la Israel likifanya operesheni huku kukiwa na mzozo unaoendelea kati ya Israel na Hamas, karibu na mpaka wa Israel na Gaza Aprili 5, 2024. REUTERS.
Gari la kijeshi la Israel likifanya operesheni huku kukiwa na mzozo unaoendelea kati ya Israel na Hamas, karibu na mpaka wa Israel na Gaza Aprili 5, 2024. REUTERS.

Israel ilisema Ijumaa kuwa inachukua hatua kuwezesha ufikishaji wa misaada ya kibinadamu katika Ukanda wa Gaza, ikiwa ni pamoja na kufungua tena kivuko muhimu cha mpaka kaskazini mwa Gaza.

Hatua hizo za muda ni pamoja na kufunguliwa tena kwa kivuko cha Erez na matumizi ya bandari ya Ashdodi. Kivuko cha Erez ndicho kituo pekee cha abiria ambacho watu wanaweza kutumia kusafiri kwenda na kutoka Gaza. Wakati huo huo, usafirishaji wa misaada ya kibinadamu kwa ajili ya Gaza utashughulikiwa kupitia bandari ya Ashdod ya Israeli. Usafirishaji wa misaada ya Jordan pia utashughulikiwa huko

Msaada huu ulioongezeka utazuia janga la kibinadamu na ni muhimu ili kuhakikisha kuendelea kwa mapigano na kufikia malengo ya vita, ofisi ya waziri mkuu ilisema katika taarifa yake.

Taarifa hiyo haikufafanua juu ya idadi au aina ya vitu vya kuingizwa.

Forum

XS
SM
MD
LG