Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Novemba 15, 2024 Local time: 11:50

Mafuriko yaua watu 37 Indonesia


Eneo lililoharibiwa na mafuriko na lava katika wilaya ya Tanah Datar, magharibi mwa jimbo la Sumatra, Indonesia, Mei 12, 2024. Picha ya AFP
Eneo lililoharibiwa na mafuriko na lava katika wilaya ya Tanah Datar, magharibi mwa jimbo la Sumatra, Indonesia, Mei 12, 2024. Picha ya AFP

Watu 37 walifariki na zaidi ya dazeni hawajulikani waliko magharibi mwa Indonesia baada ya mvua kubwa kunyesha na volcano baridi kutiririka na kuharibu nyumba, barabara na misikiti, maafisa walisema Jumapili.

Mvua za msimu zilizonyesha kwa saa kadhaa na maporomoko makubwa ya matope kutokana na lava baridi kutoka kwenye mlima Marapi yamesababisha mito kuvuka kingo zake na kuingia katika vijiji vya milimani katika wilaya nne kwenye jimbo la Magharibi la Sumatra Jumamosi usiku. Mafuriko yamewakumba watu na kuzamisha nyumba zaidi ya 100 na majengo, msemaji wa Idara ya Taifa ya Majanga Abdul Muhari amesema.

Lava baridi, pia inayojulikana kama Lahar, ni mchanganyiko wa volcano na vijiwe ambavyo vinatiririka kutoka kwenye miteremko ya volcano wakati wa mvua.

Leo mchana waokoaji walitoa miili 19 kutoka kwenye kijiji kilichoathirika vibaya sana cha Canduang katika wilaya ya Agam na kupata miili mingine tisa katika wilaya jirani ya Tanah Datar, taarifa ya Idara ya Taifa na Utafutaji na Uokoaji imesema.

Forum

XS
SM
MD
LG