Rais wa Nigeria aliamuru maafisa wa usalama kutolipa fidia kwa ajili ya kuachiliwa kwa zaidi ya wanafunzi 250 wa shule ya msingi waliotekwa nyara na watu wenye silaha wiki iliyopita, waziri wa habari alisema Jumatano.
Mahakama ya Uganda Jumanne ilitupilia mbali rufaa ya kundi la kutetea haki za wapenzi wa jinsia moja lililotaka usajili wa serikali, na kuamua kwamba kundi hilo lina lengo la kuendeleza shughuli “haramu”.
Kenya imeamua kusitisha mipango ya kutuma maafisa wa polisi nchini Haiti iliyokumbwa na ghasia chini ya ujumbe wa kimataifa unaoungwa mkono na Umoja wa Mataifa, afisa mmoja mwandamizi wa serikali ya taifa hilo la Afrika Mashariki alisema Jumanne.
Waziri Mkuu wa Haiti Ariel Henry, amesema atajiuzulu baada ya kuundwa kwa baraza la mpito la uongozi ingawa wakuu wa magenge ya uhalifu wanasisitza juu ya kuhusishwa kwenye mipango yoyote ya kuunda serikali ya mpito.
Waziri wa mambo ya nje wa Israel Israel Katz Jumatatu aliliomba Baraza la Usalama la Umoja wa mataifa “kuongeza shinikizo kwa Hamas kadri iwezekanavyo” kuwaachia huru watu ilioshika mateka katika shambulio la Oktoba 7 dhidi ya Israel.
Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Angola tete Antonio amesema Jumatatu jioni kwamba Rais Paul Kagame wa Rwanda amekubali kukutana na mwenzake wa Jamhiri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa mazungumzo kuhusu hali ya usalama mkashariki ya Congo.
Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Angola Tete Antonio amesema Jumatatu kwamba Rais Paul Kagame wa Rwanda amekubali kukutana na mwenzake wa Jamhiri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa mazungumzo kuhusu hali ya usalama mkashariki ya Congo.
Chama kikuu cha upinzani nchini Burundi kilikumbwa na mgawanyiko Jumapili baada ya tawi lake kusema kuwa limemuondoa kiongozi wa chama hicho Agathon Rwasa kwa kushindwa kuunganisha pande mbili zinazolumbana.
Wapatanishi na wawakilishi wa Hamas wamepata ‘mafanikio makubwa’ kuelekea sitisho la mapigano huko Gaza, televisheni ya Misri yenye uhusiano na serikali imeripoti Jumatatu wakati mazungumzo ya Cairo yanaingia siku ya pili.
Ripoti za uchunguzi wa maiti na kitaalamu zimethibitisha kwamba kifo cha mwanasiasa wa upinzi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kilikuwa kitendo cha kujiua, mwendesha mashtaka wa mjini Kinshasa aliviambia vyombo vya habari Alhamisi.
Watu 43 walifariki na wengine kadhaa kujeruhiwa na moto ulioteketeza jengo la ghorofa saba katika kitongoji cha mji mkuu wa Bangladesh Alhamisi, maafisa walisema.
Waandaaji wa michezo ya Olimpiki ya Paris waliingia katika kijiji kipya cha wanariadha kilichoandaliwa Alhamisi katika muda ulipangwa, ikiimarisha uthabiti unaokua kwamba wataweza kuwa tayari kwa michezo hiyo kufanyika.
Vyama vya wafanyakazi nchini Guinea Jumatano vilisema kwamba vimesitisha mgomo wa kitaifa ambao ulidumaza shughuli kwa siku tatu baada ya mwanaharakati mashuhuri wa vyombo vya habari kuachiliwa huru.
Waokoaji waliopoa zaidi ya miili 20 kwenye bahari kaskazini mwa Senegal Jumatano baada ya boti iliyokuwa inasafirisha wahamiaji kuelekea Ulaya kuzama, gavana wa eneo hilo ameiambia AFP, huku hofu ikiongezeka kuhusu wahamiaji waliotoweka.
Watu 31 walifariki nchini Mali Jumanne na wengine 10 kujeruhiwa wakati basi lililokuwa linasafiri kuelekea Burkina Faso lilipoanguka kutoka kwenye daraja kusini mashariki mwa nchi hiyo, wizara ya uchukuzi ilisema.
Utawala wa kijeshi nchini Guinea Jumanne ulisema umemteua waziri mkuu mpya siku nane baada ya kuivunja serikali ya awali, huku shughuli katika mji mkuu wa Conakry zikizorota kwa siku ya pili ya mgomo wa kitaifa.
Shambulio kwenye msikiti mashariki mwa Burkina Faso liliua Waislamu kadhaa siku hiyo hiyo ambapo kulitekelezwa shambulio jingine dhidi ya waumini wa kanisa Katokili waliokuwa wamehudhuria ibada ya misa, vyanzo vya usalama na wakazi wa eneo hilo waliiambia AFP Jumatatu.
Raia 15 waliuawa na wengine wawili kujeruhiwa katika shambulio la kigaidi kwenye kanisa katoliki wakati wa ibada ya Jumapili kaskazini mwa Burkina Faso, afisa kwenye kanisa hilo alisema.
Wagombea wengi katika uchaguzi ulioahirishwa nchini Senegal na kundi kubwa la jumuiya za kiraia kwa pamoja wamesema siku ya Ijumaa kuwa, hawatashiriki katika mazungumzo yaliyopendekezwa na Rais Macky Sall kuamua tarehe ya upigaji kura ambao aliuahirisha mapema mwezi huu.
Pandisha zaidi