Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 06:38

Waislamu kadhaa wauawa nchini Burkina Faso katika shambulio dhidi ya msikiti


Map of Burkina Faso
Map of Burkina Faso

Shambulio kwenye msikiti mashariki mwa Burkina Faso liliua Waislamu kadhaa siku hiyo hiyo ambapo kulitekelezwa shambulio jingine dhidi ya waumini wa kanisa Katokili waliokuwa wamehudhuria ibada ya misa, vyanzo vya usalama na wakazi wa eneo hilo waliiambia AFP Jumatatu.

Mashambulizi hayo mawili yalifanyika siku ya Jumapili katika maeneo tofauti ya nchi hiyo ambayo imekumbwa na miaka kadhaa ya uasi mbaya wa wanamgambo wa kiislamu.

“Watu wenye silaha walishambulia msikiti huko Natiaboani Jumapili nyakati za alfajiri, na kuua watu kadhaa”, chanzo cha usalama kimesema.

Mkazi wa eneo hilo ameiambia AFP kwa njia ya simu kwamba “Waathirika wote walikuwa Waislamu, wengi wao wakiwa wanaume waliokuja kushiriki sala ya alfajiri.”

Chanzo kingine kilisema “magaidi waliingia ndani ya mji mapema asubuhi. Walizingira msikiti na kuwaua waumini waliokuwa wamekusanyika kwa ajili ya sala ya kwanza ya siku.”

Forum

XS
SM
MD
LG