Sall anapamba na ongezeko la wito wa kumtaka atangaze siku ya uchaguzi wa rais baada ya kuuahirisha ghafla uchaguzi wa Februari 25 na kusababisha mgogoro wa kisiasa kwa wiki kadhaa.
Lakini katika majojiano ya television siku ya Alhamisi jioni, hakuzungumzia uamuzi wa kutaja tarehe mpaka baada ya mazungumzo na wanasiasa na watendaji wa kijamii, yanayotarajiwa kuanza Jumatatu.
Amesema anatarajia kufikia makubaliano ifikapo Junanne jioni.
“Tunapinga mapendekezo ya mdahalo na tunataka tarehe ipangwe kabla ya Aprili 2” Boubacar Camara mmoja wa kundi hilo la wagombea 16 aliwaambia waandishi wa habari siku ya Ijumaa.
Sall alisisitiza wakati alipoonekaka kwenye televisheni kuwa mamlaka yake itafikia hatima ya uongozi wake kama ilivyopangwa tarehe 2 Aprili.
Lakini alicha wazi swali la ni lini uchaguzi huo utafanyika. Alipobanwa , aliongeza kuwa hafikirii kama itawezekana kufanyika kabla ya April 2. Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AFP
Forum