Sall anakabiliana na kelele zinazoongezeka za kumtaka atangaze tarehe ya uchaguzi baada ya kuahirisha ghafla uchaguzi wa rais uliokuwa ufanyike Februari 25, zikiwa zimebaki wiki tatu.
Kukiwa na msukumo ndani ya nchi na nje kutaka upigaji kura ufanyike haraka, atashiriki mahojiano ya kwenye televisheni yanayojumisha vyombo vitatu vya habari saa moja jioni kwa saa za huko, ofisi ya rais imesema.
Sall alitangaza kuahirishwa kwa uchaguzi saa chache kabla ya kampeni kuanza, bunge liliunga mkono hatua hiyo licha ya upinzani mkali na kutangaza tarehe mpya ya uchaguzi katikati ya mwezi Desemba.
Upinzani umeishtumu hatua ya Sall kama “mapinduzi ya kikatiba”, wakisema chama chake kinaogopa kushindwa katika sanduku la kura.
Chanzo cha habari hii ni Shirika la habari la AFP .
Forum