Mahakama ya rufaa ilisema usajili wowote wa kundi la Sexual Minorities Uganda (SMUG) ni kinyume na maslahi ya umma na sera ya kitaifa.
Walalamishi walitaka jina hilo lisajiliwe “ kwa madhumuni ya kuimarisha haki za ngono za watu walio wachache wanaojulikana kama LGBTQ,” aliamua Jaji Catherine Bamugemereire kwa niaba ya jopo la majaji watatu.
Wanaharakati walikuwa wanakata kusajili SMUG kama kampuni ndogo ili kuiwezesha kufanya kazi kihahali nchini Uganda, ambapo vitendo vya mapenzi ya jinsia moja vimeharamishwa.
Forum