Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 16:43

Watu 31 wafariki katika ajali nchini Mali


Picha hii inaonyesha msongamano wa magari mjini Bamako, Mali
Picha hii inaonyesha msongamano wa magari mjini Bamako, Mali

Watu 31 walifariki nchini Mali Jumanne na wengine 10 kujeruhiwa wakati basi lililokuwa linasafiri kuelekea Burkina Faso lilipoanguka kutoka kwenye daraja kusini mashariki mwa nchi hiyo, wizara ya uchukuzi ilisema.

Ajali hiyo ilitokea nyakati za saa kumi na moja jioni kwenye daraja linalovuka mto Bagoe, wizara hiyo iliongeza.

“Basi lililokuwa linatokea wilaya ya Kenieba kuelekea Burkina Faso lilianguka kutoka kwenye daraja. Inawezekana kuwa sababu ni dereva kushindwa kudhibiti gari,” wizara hiyo ilisema katika taarifa.

Ajali za magari hutokea mara kwa mara nchini Mali, ambako barabara nyingi na barabara kuu kadhalika magari yapo katika hali mbovu.

Mapema mwezi huu, watu 15 walifariki na wengine 46 kujeruhiwa wakati basi lililokuwa linaelekea katika mji mkuu Bamako lilipogongana na lori katikati mwa Mali.

Forum

XS
SM
MD
LG