Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 14:00

Rais wa Senegal atangaza msamaha wa jumla kwa wapinzani wa kisiasa


Rais wa Senegal Macky Sall
Rais wa Senegal Macky Sall

Shambulio kwenye msikiti mashariki mwa Burkina Faso liliua Waislamu kadhaa siku hiyo hiyo ambapo kulitekelezwa shambulio jingine dhidi ya waumini wa kanisa Katokili waliokuwa wamehudhuria ibada ya misa, vyanzo vya usalama na wakazi wa eneo hilo waliiambia AFP Jumatatu.

Taifa hilo la Afrika Magharibi linakabiliwa na mzozo mbaya wa kisiasa katika kipindi cha miongo kadhaa baada ya Sall kuahirisha gafla uchaguzi wa rais wa Februari 25 saa chache kabla ya kampeni ya uchaguzi huo kuanza.

Sall ameitangaza hatua hiyo ya msamaha kama njia ya kuiunganisha nchi, baada ya msururu wa maandamano kuua watu kadhaa katika miaka mitatu iliyopita.

Mamia ya wapinzani, au zaidi ya wapinzani 1,000 kulingana na makundi ya haki za binadamu, walikamatwa tangu mwaka wa 2021 kufuatia mvutano wa kuwania madaraka kati ya kiongozi wa upinzani Ousmane Sonko na serikali.

Sonko na mgombea wa chama chake, Bassirou Diomaye Faye wanafungwa jela.

“Katika ari ya maridhiano ya kitaifa, nitawasilisha mbele ya bunge Jumatano hii katika baraza la mawaziri muswada wa msamaha wa jumla kwa vitendo vinavyohusiana na maandamano ya kisiasa yaliyofanyika kati ya 2021 na 2024,” Sall alisema Jumatatu.

Forum

XS
SM
MD
LG