“Tunataka kuwafahamisha kuhusu shambulio la kigaidi ambalo lililenga jamii yetu ya kikatoliki katika kijiji cha Essakane Februari 25, wakati waumini walikuwa wamekusanyika kwa ajili ya ibada ya Jumapili,” kasisi wa dayosisi ya Dori, Jean Pierre Sawadogo alisema katika taarifa iliyowasilishwa kwa shirika la habari la AFP.
Idadi ya awali ni ya watu 15 waliouawa na wawili waliojeruhiwa, aliongeza.
Akitoa wito wa amani na usalama nchini Burkina Faso, Sawadogo alilaani “wale wanaozidi kusababisha vifo na uzuni nchini.”
Kijiji cha Essakane ambako shambulio hilo lilifanyika, kinapatikana katika eneo linalojulikana kama “mtaa wa mipaka mitatu” kaskazini mashariki mwa nchi, karibu na mipaka ya pamoja kati ya Burkina Faso, Mali na Niger.
Ni shambulio la hivi karibuni katika msururu wa vitendo vya kikatili vinavyodaiwa kutekelezwa na wanamgambo wa kiislamu katika eneo hilo, baadhi ya vitendo hivyo vikilenga kanisa za Kikritso huku wanamgambo wengine wakihusika katika utekaji nyara wa wanadini.
Forum