Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 17:43

Kiongozi mkuu wa upinzani nchini Burundi aondolewa na wapinzani wake


Kiongozi wa upinzani nchini Burundi Agathon Rwasa
Kiongozi wa upinzani nchini Burundi Agathon Rwasa

Chama kikuu cha upinzani nchini Burundi kilikumbwa na mgawanyiko Jumapili baada ya tawi lake kusema kuwa limemuondoa kiongozi wa chama hicho Agathon Rwasa kwa kushindwa kuunganisha pande mbili zinazolumbana.

Rwasa aliondolewa kwenye uongozi wa chama cha National Freedom Council (CNL) katika kongamano la chama kaskazini mwa nchi, vyanzo kutoka chama hicho na mashahidi wamesema.

Nafasi ya kiongozi huyo wa zamani wa kundi la waasi mwenye umri wa miaka 60 imechukuliwa na Nestor Girukwishaka.

Chama cha CNL ambacho kilianzishwa mwaka wa 2019, kilisimamishwa mwaka jana na serikali ya Burundi ikikituhumu “kutotii sheria”.

Wakosoaji wanasema hatua hiyo ya wizara ya mambo ya ndani ni juhudi za kukandamiza upinzani kabla ya uchaguzi wa bunge wa 2025 na inaweza kuirejesha nchi hiyo kwenye mzozo wa kisiasa.

Katibu mkuu wa chama Simon Bizimungu amelaani kuondolewa kwa Rwasa akisema ni kinyume na katiba ya chama chao.

“Huu ni ukiukaji wa kifungu cha 47 cha sheria za chama ambacho kinasema kwamba ni rais na mwakilishi halali pekee ndiye anaruhusiwa kuitisha mkutano wa aina hiyo,” Bizimungu ameliambia shirika la habari la AFP.

Bizimungu amemshtumu waziri wa mambo ya ndani Martin Ninteretse kwa kukataa kumruhusu Rwasa kuandaa mkutano mkuu wa chama tarehe 2 Machi, lakini “ametoa ruhusa kwa kundi dogo la wapinzani kufanya mkutano haramu na kutupokonya chama.”

Forum

XS
SM
MD
LG