Jaji mmoja wa Haiti amemshutumu mke wa rais wa zamani kwa kuhusika na mauaji ya mume wake Juvenal Moise ambaye wakati huo alikuwa rais wa nchi.
Wanamgambo waliua watu 15 mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika jimbo la Ituri, vyanzo katika eneo hilo vilisema Jumapili, likiwa shambulio la pili chini ya wiki moja.
Kiongozi wa upinzani wa Russia Alexey Navalny, aliyefariki katika gereza la Arctic Ijumaa, alitumia ushawishi wa mitandao ya kijamii and kuonyesha kuchoshwa na utawala wa Kremlin na hivyo kupanda kufikia umaarufu.
Israel Alhamisi ilipeleka wanajeshi katika hospitali ya Gaza ambako imesema huenda mateka wanashikiliwa humo, huku madaktari wakionya kuwa kituo hicho muhimu cha kutoa matibabu kinafanya kazi katika mazingira magumu sana.
Mawaziri wa Burkina Faso, Mali na Niger walikutana katika mji mkuu wa Burkina Faso Alhamisi kujadili kuunda shirikisho, kulingana na mwandishi wa shirika la habari la AFP.
Mahakama ya katiba nchini Senegal Alhamisi ilibatilisha uamuzi wa kuahirisha uchaguzi wa rais uliopangwa kufanyika mwezi huu, hatua ambayo iliitumbukiza nchi hiyo katika mzozo mbaya kwa miongo kadhaa.
Mawakili wa Burkina Faso Alhamisi walisitisha shughuli zao na kusababisha kisimamishwa kwa kesi kwenye mahakama nyingi, wakitoa wito kuachiliwa mara moja kwa mwenzao aliyetekwa nyara mwishoni mwa Januari
Kevin Kang’ethe, mshukiwa wa mauaji ya mwanamke mmoja hapa Marekani, Jumatano alifikishwa mahakamani mjini Nairobi, na Jaji akaamuru azuiliwe kwenye gereza moja mjini humo, baada ya kukamatwa akiwa kwenye nyumba ya ndugu yake.
Rais wa Russia Vladimir Putin Jumatano alisema anamshukuru mtangazaji wa chombo cha habari cha Marekani chenye msimamo mkali wa kulia Tucker Carlson kwa kufanya mahojiano naye wiki iliyopita na “ kuchukua jukumu la mpatanishi” kama raia wa nchi za Magharibi.
Wachezaji wa timu ya taifa ya soka ya Ivory Coast na kocha wao Emerse Fae walizawadiwa pesa na nyumba za kifahari katika hafla iliyosimamiwa na Rais wa nchi hiyo Jumanne kusherekea ushindi wao katika fainali ya kombe la mataifa barani Afrika.
Mashirika ya kiraia ya Senegal na upinzani waliendelea na shinikizo lao kwa Rais Macky Sall Jumatatu, mkesha wa maandamano yaliyopangwa ili kupinga kuahirishwa kwa uchaguzi wa rais wa mwezi huu, hatua ambayo tayari imesababisha machafuko mabaya kote nchini.
Rais wa Marekani Joe Biden alikutana Jumatatu na mfalme wa Jordan Abdullah kwenye White House, ukiwa mkutano wa ana kwa ana na mshirika wa muda mrefu ambaye amekuwa akikosoa vikali mashambulizi ya Israel na kutoa wito wa sitisho la mapigano.
Polisi katika mji mkuu wa Kinshasa katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo wamefyatua gesi ya kutoa machozi kuwatawanya waandamanaji ambao wamechoma matairi ya gari na bendera za Marekani na Ubelgiji karibu na ubalozi wa nchi za Magharibi na ofisi za Umoja wa Mataifa.
Polisi wa kupambana na ghasia mjini Kinshasa wamewatupia mabomu ya kutoa machozi waandamanaji wanaotaka hatua kuchukuliwa kuzia mapigano mashariki ya nchi
Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ina lengo la kurejesha adhabu ya kifo, ambayo ilisitishwa miaka 20 iliyopita, kwa wanajeshi wanaopatikana na hatia ya uhaini dhidi ya waasi wa M23, kulingana na ripoti ya baraza la mawaziri.
Polisi wa Senegal waliwafyatulia gesi ya kutoa machozi waandamanaji siku ya Ijumaa huku hasira ikiongezeka juu ya kuahirishwa kwa uchaguzi wa rais. Kifo cha kwanza kimeripotiwa katika maandamano hayo.
Jeshi la Israel limesema kwamba takriban roketi 30 zimerushwa kaskazini mwa Israel usiku wa kuamkia leo, kutoka Lebanon kufuatia shambulizi la droni la Israel lililojeruhi kamanda wa kundi la Hezbollah linaloungwa mkono la Iran, kusini mwa Lebanon.
Waandamanaji walio na hasira walikusanyika katika mji mkuu wa Haiti Jumatano wakidai kuondoka kwa Waziri Mkuu Ariel Henry.
Kocha wa Ivory Coast Emerse Fae, alielezea ushindi wa timu yake kwenda hadi fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika kuwa "kama ndoto" baada ya wenyeji hao wa michuano ya mwaka 2024 kuwalaza Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo 1-0 katika mechi ya mchujo Jumatano.
Russia imefyatua makombora na kutumia ndege zisizokuwa na rubani huko Ukraine Jumatatno katika “ shambulizi kumbwa” la alfajiri ambalo liliuwa watu watano na kujeruhi wengine zaidi ya 30, maafisa mjini Kyiv wamesema.
Pandisha zaidi