Kang’ethe alikuwa ametoroka akiwa chini ya ulinzi wa polisi nchini, kitendo ambacho kiligonga vichwa vya habari kufuatia kukamatwa kwake, akishukiwa kumuua mpenzi wake, na kuuacha mwili wake kwenye gari, lililoegeshwa kwenye uwanja wa ndege wa Boston Logan, jimbo la Massachusetts.
Kang’ethe alikamatwa na kuwekwa chini ya ulinzi mwezi Januari akisubiri kurudishwa Marekani kutokana na kifo cha Margaret Mbitu, lakini alitoroka kutoka kwa kituo cha polisi wiki iliyopita, katika mazingizra tatanishi.
Polisi walisema Kang’ethe alikuwa amejificha katika nyumba ya ndugu yake katika kitongoji kimoja cha Nairobi, ambako polisi walimkuta Jumanne jioni baada ya msako wa siku kadhaa.
Jaji alisema Kang’ethe ataendelea kuzuiliwa hadi pale ombi la mwendesha mashtaka wa serikali, la kutaka kumrejesha nchini Marekani litakaposikilizwa na mahakama na uamuzi kutolewa.
Forum