Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Oktoba 05, 2024 Local time: 07:31

Mashirika ya kiraia na upinzani wamshinikiza Rais wa Senegal kufuta hatua ya kuahirisha uchaguzi


Rais wa Senegal Macky Sall
Rais wa Senegal Macky Sall

Mashirika ya kiraia ya Senegal na upinzani waliendelea na shinikizo lao kwa Rais Macky Sall Jumatatu, mkesha wa maandamano yaliyopangwa ili kupinga kuahirishwa kwa uchaguzi wa rais wa mwezi huu, hatua ambayo tayari imesababisha machafuko mabaya kote nchini.

Uamuzi wa Sall kuahirisha uchaguzi wa Februari 25 uliitumbukiza Senegal ilio thabiti kwa miaka kadhaa katika mzozo mbaya tangu ijipatie uhuru kutoka kwa Ufaransa mwaka wa 1960, huku maandamano mabaya yakisababisha vifo vya watu watatu.

Muungano wa wanaharakati hao wa kampeni iliopewa jina la” Tulinde uchaguzi wetu”, ambao unajumuisha makundi 40 ya kiraia, kidini na kitaaluma, waliitisha maandamano mapya katika mji mkuu wa Dakar Jumanne mchana.

“Tunawaomba Wasenegal wote kuhamasishwa, tunatoa wito kwa Wasenegal wote kujitokeza na kushiriki maandamano ya amani ili kupinga kuahirishwa kwa uchaguzi, kupinga kuongezwa kwa muhula wa Rais Macky Sall,” Abdou Khafor Kandji aliwaambia waandishi wa habari, kwa niaba ya moja kati ya makundi ya muungano huo.

Forum

XS
SM
MD
LG