Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 14:23

Putin amshukuru mwandishi wa habari wa Marekani kwa mahojiano


Picha hii yaonyesha mwandishi wa habari wa zamani wa Fox News Tucker Carlson akifanya mahojiano na Rais Vladimir Putin kwenye Ikulu ya Russia, Februari 6, 2024.
Picha hii yaonyesha mwandishi wa habari wa zamani wa Fox News Tucker Carlson akifanya mahojiano na Rais Vladimir Putin kwenye Ikulu ya Russia, Februari 6, 2024.

Rais wa Russia Vladimir Putin Jumatano alisema anamshukuru mtangazaji wa chombo cha habari cha Marekani chenye msimamo mkali wa kulia Tucker Carlson kwa kufanya mahojiano naye wiki iliyopita na “ kuchukua jukumu la mpatanishi” kama raia wa nchi za Magharibi.

Mtangazaji wa zamani nyota wa kituo cha televisheni cha Fox News, Carlson alichapisha mahojiano yake ya saa mbili na Putin mjini Moscow Alhamisi iliyopita, siku chache kabla ya kumbukumbu ya miaka miwili ya uvamizi wa Russia dhidi ya Ukraine.

Katika mahojiano hayo, Putin alisema nchi za Magharibi zinapaswa kuelewa kwamba haitawezekana Russia kushindwa katika vita vya Ukraine.

“Kwa kuwa hatuwezi kuwa na mazungumzo ya moja kwa moja na nchi za Magharibi leo, inabidi nimshukuru Carlson kwa kuweza kufanya hivyo kama mpatanishi,” Putin aliwambia waandishi wa habari katika nukuu zilizosambazwa na Kremlin.

Pamoja na hivo, Putin alisema “hakuridhishwa kikamilifu” na mahojiano hayo, yakiwa mahojiano yake ya kwanza na mwandishi wa habari kutoka nchi za Magharibi tangu Russia ilipoivamia Ukraine.

Mahojiano hayo yalitizamwa mara milioni 200 kwenye mtandao wa X, uliojulikana awali kama Twitter.

Forum

XS
SM
MD
LG