Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 04:26

Burkina Faso, Mali na Niger kuunda shirikisho


Kiongozi wa kijeshi wa Burkina Faso, Kepteni Ibrahim Traore.
Kiongozi wa kijeshi wa Burkina Faso, Kepteni Ibrahim Traore.

Mawaziri wa Burkina Faso, Mali na Niger walikutana katika mji mkuu wa Burkina Faso Alhamisi kujadili kuunda shirikisho, kulingana na mwandishi wa shirika la habari la AFP.

Serikali hizo tatu za kijeshi mwezi Septemba ziliunda mkataba wa ulinzi na uchumi, muungano wa nchi za Sahel (AES).

Waziri wa ulinzi wa Burkina Faso Jenerali Kassoum Coulibaly alisema mazungumzo ya Ouagadougou ilikuwa fursa ya kuendelea kutekeleza mikataba, mikakati na taratibu na muundo wa kisheria kwa ajili ya shirikisho.

Taratibu hizo” zitaruhusu muungano wetu na shirikisho kufanya kazi kwa ufanisi na kwa furaha kubwa” ya wanainchi wa nchi hizi tatu, mwenzake wa Niger Jenerali Salifou Modi alisema.

Mawaziri wa mambo ya nje wa mataifa hayo matatu wanaunga mkono uundaji wa shirikisho kama sehemu ya lengo la muda mrefu la kuziunga nchi hizo jirani za Afrika Magharibi ndani ya shirikisho, kwenye mkutano wa mwezi Disemba katika mji mkuu wa Mali wa Bamako.

Forum

XS
SM
MD
LG