Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 15:05

Haiti: Maandamano yaliogubikwa na ghasia yashinikiza Waziri Mkuu kuachia madaraka


Maandamano nchini Haiti.
Maandamano nchini Haiti.

Waandamanaji walio na hasira walikusanyika katika mji mkuu wa Haiti Jumatano wakidai kuondoka kwa  Waziri Mkuu Ariel Henry.

Hilo limejiri baada ya Waziri Mkuu huyo kushindwa kuachia madaraka kufuatia makubaliano ya kisiasa yaliyofikiwa mwaka 2022.

Haiti imekumbwa na ghasia tangu Jumatatu huku maelfu ya waandamanaji wakikusanyika katika mji wa Port- au- Prince na kote nchini humo.

Vyombo vya habari vya ndani vinaripoti kwamba baadhi ya maandamano yamebadilika na kuwa ghasia.

Wakati huo huo waandamanaji hao wamekuwa wakipambana na polisi na takriban watu wawili walipigwa risasi na kuuwawa katika ghasia hizo.

Kwa mujibu wa makubaliano yaliyomalizika Desemba 2022 kufuatia mauaji ya rais wa Haiti Jovenel Moise mwaka 2021.

Henry alitakiwa kuitisha uchaguzi na kisha kuachia mamlaka kwa maafisa wapya waliochaguliwa February 7 mwaka 2024.

Forum

XS
SM
MD
LG