Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 04:41

Haiti yaelezea kuvunjika moyo ikisubiri jumuiya ya kimataifa kutuma vikosi vya usalama


Haiti
Haiti

Waziri wa mambo ya nje wa Haiti alitoa wito kwa jumuiya ya kimataifa Alhamisi kuharakisha mchakato wa kutumwa kwa kikosi cha kimataifa cha kulinda usalama kusaidia polisi wa kitaifa nchini mwake kukabiliana na ghasia za kikatili za magenge.

"Nimekuwa nikifika kwenye baraza la uslama la umokja wa mataifa mara kwa mara kwa karibu miaka miwili sasa, nikiweka wazi picha halisi ambayo inakuwa ya huzuni, ikizingatiwa kwamba hali ya usalama na kibinadamu inazidi kuzorota," Jean Victor Geneus aliuambia mkutano wa Baraza hilo mjini New York. "Watu wa Haiti hawawezi kuvumilia tena," aliongeza.

Geneus alisema mustakabali wa Haiti uko katika njia panda, na anatumai itakuwa mara ya mwisho, kwake yeye kuhutubia baraza hilo kabla ya kutumwa kwa kikosi cha kimataifa, ambacho kiliidhinishwa mwezi Oktoba mwaka jana.

Kenya imejitolea kuongoza ujumbe wa kikosi cha Usalama wa Kimataifa nchini Haiti na imeahidi kutoa takriban maafisa 1,000 wa polisi.

Balozi Kenya katika Umoja wa Mataifa Martin Kimani alisema mkutano wa kuzipatia nchi nafasi ya kutoa ahadi unapangwa ili kukabiliana na upungufu ya fedha na vifaa.

Bahamas, Jamaica, Antigua na Barbuda pia wameonyesha nia ya kuchangia maafisa katika kikosi hicho.

Marekani imetoa msaada wa takriban dola milioni 200, ikiwa ni pamoja na vifaa kwa ajili ya operesheni hiyo, lakini haitatuma maafisa wowote.

Forum

XS
SM
MD
LG