Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 05:31

Mkuu wa jeshi la polisi la Haiti yupo Kenya kwa mazungumzo na nchi hiyo


 Frantz Elbe, Mkuu wa Jeshi la Polisi la Haiti
Frantz Elbe, Mkuu wa Jeshi la Polisi la Haiti

Maafisa wa Kenya walisema Alhamisi kwamba Frantz Elbe, katika harakati za kutafuta ukweli, alikutana na mkuu wa polisi wa Kenya Japhet Koome siku ya Alhamisi.

Mkuu wa jeshi la polisi la Haiti aliitembelea Kenya Alhamisi, wakati mamlaka za ndani zikijiandaa kupelekwa kwa polisi wa Kenya katika taifa la Caribbean lililokumbwa na ghasia za magenge.

Maafisa wa Kenya walisema Alhamisi kwamba Frantz Elbe, katika harakati za kutafuta ukweli, alikutana na mkuu wa polisi wa Kenya Japhet Koome siku ya Alhamisi.

Elbe yuko katika ziara rasmi ya siku tatu nchini Kenya kwa majadiliano ya usalama baina ya taasisi hizo mbili za kutekeleza sheria, taarifa kutoka ofisi ya Koome ilisema. Hakuna maelezo zaidi yaliyotolewa.

Nembo ya Umoja wa Mataifa-UN
Nembo ya Umoja wa Mataifa-UN

Mwezi Oktoba, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa liliidhinisha kupelekwa kwa kikosi cha kigeni kinachoongozwa na Kenya nchini Haiti kusaidia kuleta udhibiti wa ghasia za magenge.

Zaidi ya mauaji 1,230 na utekaji nyara 701 yaliripotiwa kote nchini Haiti kuanzia Julai Mosi hadi Septemba 30, ikiwa ni mara mbili ya idadi iliyoripotiwa katika kipindi kama hicho mwaka jana, kulingana na Umoja wa Mataifa.

Forum

XS
SM
MD
LG