Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 17:06

Bunge la Kenya laidhinisha upelekaji wa polisi nchini Haiti


Polisi wa Kenya wakishika doria baada ya ghasia jiji Nairobi. Picha ya maktaba.
Polisi wa Kenya wakishika doria baada ya ghasia jiji Nairobi. Picha ya maktaba.

Wabunge nchini  Kenya Alhamisi wameidhinisha hatua  ya kupeleka maafisa polisi 1000 nchini Haiti.

Operesheni iliyoidhinishwa na Umoja wa Mataifa, kwa lengo la kulisaidia taifa hilo la Caribbean, kukabiliana na tatizo la ghasia za magenge. Mwezi Julai Kenya iliahidi kupeleka maafisa 1,000 wa polisi nchini humo, baada ya ombi la kimataifa la Haiti la maafisa wa usalama, ili kusaidia katika kukabiliana na magenge yanayolaumiwa kueneza uhalifu.

Hata hivyo mapema Oktoba chama kimoja cha upinzani nchini Kenya kiliwasilisha kesi mahakamani kikipinga upelekaji huo. Chama hicho kilidai kuwa umma haukuhusishwa kwenye maamuzi hayo, na kwamba ni wanajeshi pekee, wanaoweza kutumwa nje ya nchi kwa mujibu wa katiba.

Naibu Spika wa bunge Gladys Boss Shollei amechukua kura za wabunge, ambao wameidhinisha upelekaji huo, wakisema kwamba ni wa kikatiba, na kwamba maoni ya umma yalichukuliwa kati ya Novemba 2 na 9.

Forum

XS
SM
MD
LG