Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 16:05

Mahakama nchini Kenya yapinga uamuzi wa serikali kupeleka polisi huko Haiti.


Bodaboda ikipita pembeni mwa moshi uliotokana na mataili yaliyochomwa moto huko Port-au-Prince Agosti14, 2023. Picha na Richard PIERRIN / AFP.
Bodaboda ikipita pembeni mwa moshi uliotokana na mataili yaliyochomwa moto huko Port-au-Prince Agosti14, 2023. Picha na Richard PIERRIN / AFP.

Mahakama nchini Kenya imepinga uamuzi wa serikali kuwatuma maafisa wa polisi wa Kenya kwenda Haiti katika misheni ya kiusalma nchini humo.

Katika maamuzi yake mahakama inasema hatua hiyo ni kinyume cha sheria na kuwa baraza la kitaifa la usalama halina mamlaka ya kuwatuma polisi Haiti.

"Tamko linatolewa kuwa Baraza la Usalama la Kitaifa halina mamlaka ya kutuma maafisa wa polisi," aliamuru jaji.

Badala yake mahakama inasema baraza la usalama linaweza kuwatuma maafisa wa jeshi katika shughuli za kiusalama katika mataifa kama vile Haiti.

Mwaka jana Rais William Ruto iliidhinisha maafisa wa polisi kutoka Kenya kuongoza kikosi cha usalama nchini Haiti, katika jitihada za kuondoa makundi ya kigaidi katika taifa hilo la Caribbean ambalo limekuwa likikubwa na vita kwa muda mrefu na kupelekea vifo vya takribana raia 5,000 kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa.

Ila uamuzi huo wa Rais ulipingwa na kiongozi wa kisiasa nchini Kenya Ekuru Aukot aliyeelekea mahakani na kupinga umauzi huo wa rais wa kuwatuma takriban maafisa 1000 Haiti.

Uamuzi huu unajiri huku hata ikiwa tayari baraza la Usalama la umoja wa mataifa lilikwishaidhinisha zoezi hilo.

Forum

XS
SM
MD
LG