Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 03:55

Mahakama Kenya imewapa maafisa polisi siku 14 kumfungulia mashtaka Mackenzie


Paul Nthenge Mackenzie, kiongozi wa kundi la dini kanisa la Kiinjili la Good News International.
Paul Nthenge Mackenzie, kiongozi wa kundi la dini kanisa la Kiinjili la Good News International.

Paul Mackenzie anashutumiwa kwa vifo vya waumini wa Good News International akiwahamasisha wafunge ili "Wakutane na Yesu".

Mahakama moja nchini Kenya imewapa maafisa polisi siku 14 kumfungulia mashtaka mshukiwa kiongozi wa kundi la kidini au wamuachilie huru baada ya kumzuia kwa vifo vya mamia ya wafuasi wake.

Paul Nthenge Mackenzie ameshuhudia kuzuiliwa kwake kwa miezi tisa kukiongezewa muda mara kadhaa wakati tayari uchunguzi ukiendelea kuhusu kile kilichotokea katika msitu wa Shakahola, karibu na pwani ya Bahari ya Hindi, ambako mabaki ya miili ya binadamu iligunduliwa mwezi Aprili mwaka jana.

Dereva wa zamani wa teksi, alikamatwa Aprili 14, anatuhumiwa kuwachochea mamia ya wafuasi wake wa Kanisa la Kiinjili la Good News International kukaa na njaa hadi kufa ili “wakutane na Yesu”, kulingana na ripoti ya Seneti.

Mackenzie na wenzake wanaaminika kuwazuia wafuasi kuacha kufunga au kujaribu kukimbia kutoka msituni.

Forum

XS
SM
MD
LG