Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 16:35

Tanzania yafuta safari za ndege za kenya Airways mjini Dar es Saalam


Ndege ya Shirika la ndege la Kenya Airways
Ndege ya Shirika la ndege la Kenya Airways

Tanzania imefuta leseni ya shirika la ndege la Kenya Airways, ya safari za ndege kutoka Nairobi hadi kwenye mji mkuu  wa Dar es Salaam, mamlaka ya safari za ndege Tanzania imesema Jumatatu.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, Tanzania imesema kwamba hatua hiyo ni majibu kufuatia Kenya kuzuia ndege za mizigo za Tanzania kuingia Kenya.Kupitia taarifa, Mamlaka ya Safari za Ndege ya Tanzania, TCAA, imesema kwamba imesitisha safari za ndege za Kenya Airways kati ya Nairobi na Dar es Salaam kuanzia Januari 22 mwaka huu.

TCAA pia imeongeza kusema kwamba hatua ya Kenya kuzuia ndege za mizigo za Tanzania ni kinyume cha makubaliano ya 2016, kati ya mataifa yote mawili kuhusiana na safari za ndege. Kupitia taarifa, shirika la Kenya Airways limesema kwamba linafahamu kuhusu marufuku hiyo, na kwamba linazugumza na mamlaka husika kutoka mataifa yote mawili, ili kuhakikisha safari za ndege kati ya Nairobi na Dar es Saalam hazivurugiki.

Forum

XS
SM
MD
LG