Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 16:04

Baada ya kuzuia uingizaji mahindi Malawi yapokea unga kutoka Tanzania


Wanawake wakiwa katika shamba la mahindi katika huko Mzuzu, Kaskazini mwa malawi Aprili 19, 2016. Picha na Amos Gumulira / AFP.
Wanawake wakiwa katika shamba la mahindi katika huko Mzuzu, Kaskazini mwa malawi Aprili 19, 2016. Picha na Amos Gumulira / AFP.

Licha ya uhaba wa chakula unaoendelea, serikali ya Malawi mwezi uliopita ilipiga marufuku uagizaji wa mahindi ambayo hayajasagwa kutoka Kenya na Tanzania, kwa hofu ya kuenea ugonjwa “Necrosis” wa mahindi, au MLN.

Ili kuwasaidia Wamalawi kupata chakula, shirika la mpango wa chakula duniani (WFP) limeanza kusaga tani 30,000 za mahindi ya msaada. Serekali inasema shehena ya kwanza ya nafaka iliyosagwa inatarajiwa kufika wiki ijayo.

Cha kushangaza, mahindi ambayo WFP ilinunua na kuyasaga yanatoka Tanzania. Mahindi hayo yalishikiliwa wiki iliyopita, na kusubiri wataalam ili kuyapima kama yana ugonjwa.

Hata hivyo, mkurugenzi wa WFP wa Malawi, Paul Turnbul, aliviambia vyombo vya habari vya ndani kuwa kutokana na muda, ilikubaliwa kutofanyika vipimo vyovyote na badala yake WFP itayazsaga mahindi na kuingiza unga Malawi.

Charles Kalemba ni kamishna wa idara ya masuala ya kukabiliana na maafa ya Malawi. Ameliambia shirika la utangazaji la serikali Jumanne kwamba kuagiza unga ni salama.

Watu wakila chakula katika kijiji cha Kamkwamba
Watu wakila chakula katika kijiji cha Kamkwamba

“Tunapata unga wa mahindi kutoka Tanzania kwa sababu wizara ya kilimo haikusema hatuwezi kupata unga. Mahindi ambayo yanaweza kupandwa, ndiyo yenye tatizo. Lakini kupata unga kamili wa mahindi ni sawa.”

Wizara ya kilimo imesema ugonjwa wa mahindi unaohofiwa hauna tiba na unaweza kusababisha hasara ya asilimia 100 ya mavuno.

Mtaalamu wa ulinzi wa mazao wa Malawi, Ronald Chilumpha Ameiambia VOA kuwa hatarajii Malawi kupiga marufuku mahindi kutoka Tanzania.

“Ugonjwa wa mahindi umekuwepo Afrika Mashariki toka 2012. Malawi imekuwa katika hali ya tahadhari kuhusu uwezekano wa kuwepo kwa ugonjwa huo. Ninaamini kuwa haya ni maswala ya kisayansi ambayo yanaweza kujadiliwa kisayansi na kufikia makubaliano.” amesema

Serikali ya Malawi inakadiria kuwa watu milioni 4.4, takriban robo ya wakazi wa Malawi, watakabiliwa na uhaba wa chakula katika kipindi cha miezi mitatu ijayo.

Shamba la mahindi lililiharibiwa na ma mafuriko Kusini mwa malawi. Picha na
Shamba la mahindi lililiharibiwa na ma mafuriko Kusini mwa malawi. Picha na

Uhaba wa chakula unatokana na athari za kimbunga Freddy, ambacho kilisomba maelfu ya hekta za mazao karibu mwaka mmoja uliopita.

Takwimu za serikali zinaonyesha kuwa akiba ya mahindi katika hifadhi ya kimkakati ya kitaifa imeshuka hadi tani 68,000, kutoka 100,000 chini ya mahitaji ya kukabiliana na njaa katika taifa hilo la kusini mwa Afrika.

Mkurugenzi wa WFP wa kanda ya kusini mwa Afrika, Menghestab Haile alikutana na rais wa Malawi Lazarus Chakwera Jumanne. Aliwaambia waandishi wa habari kuwa nchi nyingine kadhaa za Afrika pia zinakabiliwa na hali ya njaa.

Wakati huo huo, serekali ya Malawi imetangaza kuagiza mahindi kutoka Afŕika Kusini.

Forum

XS
SM
MD
LG