Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Novemba 22, 2024 Local time: 11:02

Uganda kuondolewa kwenye orodha ya nchi dhaifu dhidi ya ulanguzi wa fedha


Rais wa Youganda akizungumza katika mkutano wa kibiashara wa kikanda uliofanyika Nairobi April 8,2022. Picha na Tony KARUMBA / AFP.
Rais wa Youganda akizungumza katika mkutano wa kibiashara wa kikanda uliofanyika Nairobi April 8,2022. Picha na Tony KARUMBA / AFP.

Baada ya kufuata viwango vya kimataifa, Uganda inatarajia kuondolewa katika orodha ya ‘Grey List’ ya nchi dhaifu katika sheria za kuzuia ulanguzi wa pesa haramu na ufadhili wa ugaidi mapema mwaka ujao

Ripoti ya shirika la kimataifa la vita dhidi ya fedha haramu na ufadhili wa ugaidi lenye makao yake Paris, Ufaransa, imesema Uganda imekamilisha mageuzi ya kupambana na ulanguzi wa fedha na kukabiliana na ufadhili wa kanuni za ugaidi na inatarajia kuondolewa katika orodha hiyo mwezi Februari mwaka ujao.

Akizungumza na Sauti ya Amerika, Samuel Were Wandera ambaye ni mkurugenzi wa Mamlaka ya Ujasusi wa Kifedha ulioanzishauchunguzi kwa ulanguzi wa fedha nchini Uganda alisema “Viwango vilivyowekwa vinahitaji kila nchi kuweka mifumo ya viwango vya kupambana na ulanguzi wa fedha, kulikuwa na mapungufu machache ya kimkakati ambayo serikali ilikubali kuyashughulikia,”

“Wawakilishi wa FATF walikuwa hapa hivi karibuni na tukafanya mikutano kadhaa kujaribu kudhihirisha na tunatarajia kwamba mnamo Februari mwaka ujao Uganda itaondoka kwenye orodha ya ‘Grey List’ alisema Wandera.

Ikiwa nchi iko kwenye orodha hiyo, ina udhaifu wa kuzuia ulanguzi wa pesa na ufadhili wa ugaidi na kwa hivyo ni tishio kwa mfumo wa kifedha wa kimataifa.

Nchi iliyoorodheshwa inapata shida kufanya miamala ya kifedha ndani na nje ya nchi, kulingana na Samuel Wandera na kuongezea imeathiri uwekezaji wa moja kwa moja wa Uganda jambo ambalo limeathiri uchumi wa nchi hiyo.

“Nchi hupoteza kati ya asilimia mbili na asilimia tatu ya jumla ya pato la nchi, Uganda inapoteza kati ya shillingi trillioni nne na tisa kila mwaka ambapo ni sawa na dola billioni moja kwa ulanguzi wa fedha kila mwaka, kwa hivyo ulanguzi wa pesa ni tishio kwa uchumi.” Alisema.

Uganda iliorodheshwa kwenye orodha hiyo mapema mwaka 2020 kwa tuhuma kwamba nchi hiyo ilikuwa haijaziba mianya ya kupambana na ulanguzi wa fedha haramu na kupambana na ufadhili wa utekelezaji wa ugaidi

Kwa sasa Uganda ni nchi ya nne kwenye orodha katika nchi za Afrika Mashiriki mbapo Tanzania, Sudan Kusini na DRC ziko kwa orodha hiyo.

Forum

XS
SM
MD
LG