Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 17:42

Bibi na wajukuu zake wachomwa moto Uganda


Wanajeshi wa vikosi vya jeshi la ulinzi Uganda (UPDF) wakifanya doria dhidi ya waasi wa ADF huko Mukakati Desemba 14, 2021 Picha na AFP.
Wanajeshi wa vikosi vya jeshi la ulinzi Uganda (UPDF) wakifanya doria dhidi ya waasi wa ADF huko Mukakati Desemba 14, 2021 Picha na AFP.

Wanamgambo kutoka kundi la wanajihadi la Allied Democratic Forces (ADF) limemchoma moto bibi na wajukuu zake wawili mpaka kufa siku ya Krismasi huko magharibi mwa Uganda, maafisa wa eneo hilo wamesema.

Shambulio hilo lililotokea katika kijiji kwenye wilaya ya Kamwenge, limekuja wiki moja kufuatia mauaji ya watu kumi yaliyofanywa na ADF katika eneo hilo, kundi hilo baya lina mahusiano na kundi la Islamic State.

Kamishna mkaazi wa wilaya ya Kamwenge Isiah Byarugaba ameliambia shirika la habari la AFP kuwa washambuliaji waliichoma moto nyumba wakati waathirika wakiwa ndani.

“Waasi wa ADF wamewaua watu watatu, mwanamke mzee na wajukuu zake wawili. Waliunguzwa wakiwa ndani ya nyumba yao jana usiku” alisema.

Jeshi na polisi wanawafuatilia washambuliaji, aliongeza

Desemba 19, waasi wa ADF waliwaua watu 10 katika eneo la kibiashara la Kamwenge, wilaya n iliyoko karibu na mpaka wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambako ni ngome ya kundi hilo la waasi.

ADF inashutumiwa kufanya mauaji ya maelfu ya watu huko DRC katika miaka ya hivi karibuni na kufanya mashambulizi katika mpaka ulioko kwenye ardhi ya Uganda.

Forum

XS
SM
MD
LG