Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 12:44

Hali ya ushindani yaendelea DRC kukiwa na mivutano mikubwa kati ya wagombea


Mfumo wa kupiga kura kwa kutumia mashine nchini DRC
Mfumo wa kupiga kura kwa kutumia mashine nchini DRC

Siku chache kabla mwisho wa kampeni za uchaguzi, bado hali ya ushindani inaendelea Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, DRC, huku kukiwa na mivutano mikubwa kati ya wagombea.

please wait

No media source currently available

0:00 0:04:11 0:00

Wagombea wanaendelea katika hali ya ushindani mkali kujaribu kuwashawishi wapiga kura huku wakinadi sera zao.

Na baadhi yao wakishutumiana kwa uongozi mbaya au ukabila na hali ya sintofahamu kwa baadhi ya wapiga kura ambao wanasubiri kadi mpya za uchaguzi ambazo zitawasaidia kushiriki zoezi la upigaji kura.

Kama inavyoonekana wakati huu nchini DRC, picha na mabango ya wagombea yamebandikwa katika sehemu mbalimbali haswa maeneo ya umma. Wagombea wengine wakizunguka wakipiga muziki ili kuwavutia wakaazi waweze kuwachagua.

Mwanahabari Hassan Murhabazi

Hassan Murhabazi ni mwanahabari wa zamani anayegombea kwa tiketi ya chama cha Upinzani cha Ensemble, anaelezea:

Murhabazi, Mgombea ubunge wa Jimbo: "Mimi ni namba 260. Wagombea wengine wameiba pesa za serikali walipokuwa madarakani, na kuna wengine wanaotumia hizohizo pesa za serikali wakiwa bado madarakani kwa kufanya kampeni yao. Sasa sisi tuliotoka katika asasi za kiraia tuna shida kukutana uwanjani na watu wanaotumia mfuko wa serikali."

Licha ya changamoto, wagombea urais, ubunge wa kitaifa na majimbo na hata wagombea udiwani wanafanya kampeni zao kujaribu kuwashawishi mamilioni ya watu wa Kongo kupiga kura na kuwachagua wao.

Rais Felix Tshisekedi

Tangu kuanza kampeni yake, Rais Felix Tshisekedi anayemaliza muhula wa kwanza amewalaumu baadhi ya wagombea wenzake bila kuwataja majina kwa kile alichodai wanatuwa na nchi za kigeni, na wengine wanaunga mkono machafuko ya mashariki mwa Congo.

Rais Felix Tshisekedi
Rais Felix Tshisekedi

Akiwa pia mgombea ubunge wa kitaifa mjini Bukavu, Profesa Pascal Isumbisho ni mwanachama wa chama cha LGD cha Waziri Mkuu wa zamani Augustin Matata Ponyo, anaelezea masikitiko yake.

Mgombea Profesa Isumbisho

Profesa Pascal Isumbisho, Mgombea ubunge wa kitaifa: “Wote waliokubalika na Mahakama ya kikatiba ni raia wa Congo, sasa kwa msingi gani anaendelea kudai kuwa miongoni mwa wagombea kuna wageni? Mwenyewe kila mara anasema kwamba waasi wanasindikizwa na Rais Kagame, sasa leo anageuza kwamba ni raia wa Congo wanaowasindikiza? Ni nani aliyemkaribisha Kagame mjini Kinshasa; Felix. Nani aliyesema kwamba Kagame na Museveni ni ndugu zake? Felix Tshisekedi. Tunacho taka sisi ni: twende kwenye uchaguzi. Mimi ni namba 252 mjini Bukavu.”

Kutoka kushoto ni Rais Paul Kagame wa Rwanda, mwenzake Yuweri Museveni wa Uganda, Joao Lourenco wa Angola na Felix Tshisekedi wa DRC walipokutana Katuna/Gatuna, katika mpaka wa Rwanda na Uganda , Februari 21, 2020. (Twitter/Yuweri Museveni)
Kutoka kushoto ni Rais Paul Kagame wa Rwanda, mwenzake Yuweri Museveni wa Uganda, Joao Lourenco wa Angola na Felix Tshisekedi wa DRC walipokutana Katuna/Gatuna, katika mpaka wa Rwanda na Uganda , Februari 21, 2020. (Twitter/Yuweri Museveni)

Upinzani Wakosolewa

Lakini pia wadadisi wa mambo wanaukosoa upinzani kwamba unachukua muda mrefu kuukosoa utawala uliopo bila kueleza wazi njia mbadala za kuleta mabadiliko yaliyo tarajiwa na raia wa Congo. Edouard Makala ni mwanachama wa chama tawala cha UDPS mjini Bukavu.

Makala, Mwanachama cha UDPS/Bukavu: “Inatokana na kampeni inavyofanyika wakati ambapo nchi iko ndani ya vita, na kuna wagombea ambao hata siku moja hawajawahi kuitaja Rwanda kuwa inahusika. Lakini pia wakati wa kampeni za uchaguzi hata Ulaya, Amerika na kadhalika... wagombea wanapokuwa ndani ya kampeni mara kwa mara kuna maneno wanabadilishana.

Ni jambo la kawaida ambalo halitakuwa na madhara yoyote kwavile baada ya uchaguzi raia wa Congo wataishi tena kwa utulivu pamoja.”

Tume Huru ya Kitaifa ya Uchaguzi, CENI

Katika barua yake ya Desemba 5, Tume Huru ya Kitaifa ya Uchaguzi CENI ilimwandikia Rais Félix Tshisekedi kumfahamisha kwamba bado inatafuta njia za kupeleka vifaa vya uchaguzi kwenye maeneo mbali mbali ya nchi.

Mkuu wa Tume Huru ya Uchaguzi ya Taifa Denis Kadima (kulia), Kinshasa, 20 Oktoba 2023. (CENI RDC)
Mkuu wa Tume Huru ya Uchaguzi ya Taifa Denis Kadima (kulia), Kinshasa, 20 Oktoba 2023. (CENI RDC)

Kiongozi wa tume ya uchaguzi alitoa wito wa dharura kwa Rais Félix Tshisekedi kuomba Antonov nne na helikopta kumi ili kuwasilisha vifaa vya uchaguzi katika baadhi ya maeneo ya Congo.

Mbali na changamoto hiyo ya kusafirisha vifaa, Tume ya uchaguzi CENI ilionyesha kuwa ilitegemea kupatiwa dola milioni 170 kutoka kwa serikali ili kukamilisha ufadhili wa shughuli hii ya uchaguzi. Kiasi hiki ni salio la jumla ya dola milioni 300.

Vifaa vya Kupiga Kura Vyawasili Nchini

Kulingana na CENI, tani kadhaa za vifaa vya kupigia kura tayari viko nchini, na shehena za mwisho zingepaswa kuondoka huko nje ya nchi kabla ya Desemba 10 na kufikishwa katika maeneo tofauti kote nchini DRC tayari kwa ajili ya uchaguzi.

Mgombea Urais wa Upinzani Moise Katumbi

Mgombea urais wa upinzani Moïse Katumbi Chapwe amesema yuko tayari kutoa mchango wake kwa kutoa ndege hizo zinazo hitajika kwa nia ya kufanikisha uchaguzi tarehe 20 Disemba. Mwanasiasa huyo wa upinzani ameandika hivyo kwenye akaunti yake ya mtandao wa X akihisi kwamba ombi hilo la CENI lisiwe kisingizio cha kutoandaa uchaguzi uliopangwa Desemba 20.

Mgombea Urais wa Chama cha Upinzani Moise Katumbi
Mgombea Urais wa Chama cha Upinzani Moise Katumbi

Shirika la habari la Congo ACP limetangaza kwamba Kinshasa na Luanda ziliamua kupeleka ndege na helikopta za Angola kupeleka vifaa hivyo kote Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Msimamizi wa Tume ya Uchaguzi, CENI

Hata hivyo, Tume Huru ya Kitaifa ya Uchaguzi (CENI) inaendelea kuhakikishia kwamba uchaguzi utafanyika D20. Denis Kadima ni msimamizi wa Tume ya Uchaguzi Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, anaeleza:

Denis Kadima, Msimamizi wa CENI DRC: Tuna uwezo mkubwa wa kuifanya kazi kwaharaka, lakini ikiwa hatuna pesa za kutosha tutatafuta njia nyingine za usafirishaji wa vifaa, wafanyakazi. Inaweza kuchukua muda mrefu zaidi lakini haijalishi inachukua muda gani sisi daima tutajitahidi kuheshimu kalenda yetu”

Floribert Anzuluni ni mgombea Urais namba tano atoa onyo kwa raia wa Congo

Anzuluni, Mgombea Urais DRC anasema: “Ikiwa uchaguzi utafanyika desemba 20, kwa hali yoyote ile tutaenda tu, hata kadi zetu za kupigia kura zifutike tutaenda tu. Inabidi kwenda kwenye uchaguzi na hatuwezi kubali tena waibe kura zetu. Ikiwa tunataka mabadiliko nilazima tubadili viongozi.”

Mgombea Urais Denis Mukwege

Mgombea wa Urais Denis Mukwege akiwasalimia wafuasi wake huko katika uwanja wa ndege wa Kavumu-Bukavu wakati akiwasili kufanya kampeni Bukavu, makao makuu ya mkoa wa kusini Kivu, Mashariki ya DRC, Novemba 25, 2023.
Mgombea wa Urais Denis Mukwege akiwasalimia wafuasi wake huko katika uwanja wa ndege wa Kavumu-Bukavu wakati akiwasili kufanya kampeni Bukavu, makao makuu ya mkoa wa kusini Kivu, Mashariki ya DRC, Novemba 25, 2023.

Katika barua yake ya hivi majuzi, mgombea urais Denis Mukwege ameishutumu mamlaka kumzuia kufanya kampeni yake. Anasikitika kwamba mabango yake yameondolewa katika majimbo tofauti ya DRC na kumepita siku chache huko Goma, vibonzo vya kampeni vyenye picha zake vilikatwa kwa msumeno kwa amri ya Meya wa jiji hilo kwa kutarajia kuwasili kwa Rais anayemaliza muda wake. Pia anasema katika viwanja vya ndege kadhaa, utawala umenunua mafuta ili kuzuia usafiri wa ndege zingine zilizobeba wagombea wengine wa upinzani kuendesha kampeni zao za uchaguzi.

Kwa mara kadhaa asasi za kiraia zimeshotea pia zimeshutumu kwamba wagombea Urais hawafikiye vyombo vya habari vya umma kwa usawa kulingana na sheria ya uchaguzi. Asazi za kiraia zinaonya kuhusu kampeni ya uchaguzi yenye utulivu.

Imetayarishwa na mwandishi wetu Mitima Delachance, Bukavu, DRC

Forum

Zinazohusiana

XS
SM
MD
LG