Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 17:24

Uchaguzi Mkuu DRC: Tume ya Uchaguzi yaandikisha takriban wapiga kura zaidi ya milioni 43


Denis Kadima (G1),Afisa wa Tume ya Uchaguzi (CENI) akiandikisha wapiga kura. (Twitter/CENI RDC)
Denis Kadima (G1),Afisa wa Tume ya Uchaguzi (CENI) akiandikisha wapiga kura. (Twitter/CENI RDC)

Tume ya uchaguzi nchini Congo imeandikisha takriban wapiga kura zaidi ya milioni 43 kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa mwezi Desemba ikilinganishwa na milioni 40.4 katika uchaguzi uliopita , imesema jumatatu huku wengine upande wa upinzani wakidai kulikuwa na kasoro.

Mvutano wa kisiasa umezidi kuongezeka Drc kabla ya upigaji kura wa desemba 20 ambapo rais Felix Tshisekedi anatarajia kuwania tena muhula wa pili.

Vikosi vya usalama vilifyatua gesi ya kutoa machozi katika maandamano ya kuipinga serikali mwishoni mwa wiki huku waandamanaji wakirejea malalamiko ya wagombea wa upinzani juu ya uchelewesho na hitilafu katika maandalizi ya kuelekea upigaji kura.

Waandamanaji katika taifa hilo lenye watu takriban milioni 95 pia walikasirishwa na kupanda kwa gharama za maisha na ongezeko la ghasia upande wa mashariki , ambako makundi ya wanamgambo yenye silaha wanagombea ardhi na rasilimali za madini.

Ukosefu wa usalama umepelekea ugumu wa kujiandikisha wapiga kura katika maeneo kadhaa . CENI imesema inatafuta suluhisho ili kuwaandikisha.

Forum

XS
SM
MD
LG