Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 21:36

Tshisekedi:mzozo mashariki mwa DRC unaweza kuvuruga maandalizi ya uchaguzi


Felix Tshisekedi, Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, akihudhuria ufunguzi wa Mkutano wa 36 wa Bunge la Umoja wa Afrika huko Addis Ababa, Ethiopia Februari 18,2023. REUTERS
Felix Tshisekedi, Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, akihudhuria ufunguzi wa Mkutano wa 36 wa Bunge la Umoja wa Afrika huko Addis Ababa, Ethiopia Februari 18,2023. REUTERS

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Felix Tshisekedi alisema Jumatatu kwamba mzozo na waasi mashariki mwa nchi hiyo unaweza kuvuruga maandalizi ya uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika Desemba 20.

Tume ya uchaguzi ya Congo ilianza kuandikisha wapiga kura Februari 17 katika jimbo la Kivu Kaskazini, ambalo baadhi ya sehemu zake zinakaliwa na waasi wa M23, wanamgambo wanaoongozwa na Watutsi ambao wamekuwa wakifanya mashambulizi dhidi ya wanajeshi wa Congo kwa karibu mwaka mmoja.

Mapigano hayo yamesababisha maelfu ya watu kuyahama makazi yao, jambo ambalo limezua wasiwasi kuhusu uwezo wa jimbo hilo kuandaa uchaguzi wa wabunge na rais baadaye mwaka huu.

“Kuendelea kwa vita mashariki mwa nchi yetu kuna kunahatarisha mchakato wa uchaguzi, ambao tayari unaendelea, kutokana na kuhama kwa watu wengi kutoka katika maeneo ya mapigano, ukosefu wa usalama na kutoweza kufikiwa kwa maeneo haya," Tshisekedi aliuambia mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Binadamu.

XS
SM
MD
LG