Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 06:15

Kuelekea uchaguzi mkuu DRC: Banyamulenge walamikia kampeni za chuki


Wafuasi wa upinzani wakiwa katika kampeni za uchaguzi katika mji wa Goma ulioko Kivu Kaskazini, Desemba 6, 2018. Picha na shirika la habari la REUTERS/Samuel Mambo.
Wafuasi wa upinzani wakiwa katika kampeni za uchaguzi katika mji wa Goma ulioko Kivu Kaskazini, Desemba 6, 2018. Picha na shirika la habari la REUTERS/Samuel Mambo.

Kundi la raia wa Kongo wenye asili ya kitutsi wamekuwa wakilindwa na polisi wenye silaha wakati wakijiandikisha kupiga kura katika mji wa Nyangezi ulioko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, huku mmoja wao alilieleza kuwa kampeni za ghasia zimelenga kuwaengua katika uchaguzi ujao.

Mpiga kura wa mara ya kwanza alijiyejitokeza katika kituo cha uandikishaji akiwa na majeraha usoni na kukikumbatia kiganja chake baada ya kudaiwa kupigwa kwa fimbo na mawe na vijana wakati alipokuwa akielekea kwenye kituo cha kujiandikisha .

"Walikuwa wakisema, 'nenda kwenu'," alisema Philippe Ruhara, mwenyeji wa eneo hilo na pia ni mwakilishi wa Watutsi wanaoishi katika jimbo la Kivu Kusini wanaojulikana kama Banyamulenge.

Alisema watu katika jumuiya yake wamekuwa wakipokea vipeperushi vikiwaonya kutopiga kura – ikiwa ni sehemu ya kampeni ya chuki ambayo pia imeshuhudia makundi ya vijana wa kiume waliokusanyika katika vituo vya uandikishaji kuwazuia wapiga kura wenye asili ya Kitutsi.

Kwingineko katika viwanja vya shule zilizoko katika maeneo ya Bukavu mji kuu wa jimbo, kundi la vijana wa kiume wamekuwa wakipiga kelele na kumdhihaki mwanabmmebmmoja wa kitutsi ambaye alifika kujiandikisha kupiga kura, kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters.

Kwa muda mrefu watutsi walio wachache wanaoishi huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wamekuwa wakibaguliwa kutokana na uhusiano wao na jamii ya Watutsi walioko Rwanda.

Kongo inaishutumu Rwanda kwa kutaka kuyumbisha maeneo yake ya mashariki mwa nchi, hivi karibuni ilidai kuwa Rwanda imekuwa ikiunga mkono mashambulizi ya kundi la waasi la M23 ambalo limesababisha maelfu ya watu kuhama makazi yao. Rwanda inakanusha madai hayo ya kuliunga mkono kundi hilo lenye silaha.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari ka Reuters

XS
SM
MD
LG