Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 03:31

Vijana wa DRC wahamishwa kuhusu umuhimu wa uzalendo na amani kwenye mchakato wa uchaguzi


Vijana wakipewa elimu ya kijamii, Kivu Kusini. Februari 28, 2023.
Vijana wakipewa elimu ya kijamii, Kivu Kusini. Februari 28, 2023.

Shirika lisilo la kiserikali, DRC, linaloitwa Karibu Jeunesse Nouvelle, limechukua jukumu kuhamasisha vijana wa jimbo la Kivu kusini kuhusu uzalendo pamoja na jukumu la vijana katika kudumisha utulivu wakati wa uchaguzi.

Kupitia michezo ya kuigiza, muziki, vibonzo na kadhalika, shirika hilo limekusanya mamia ya vijana kutoka maeneo mbalimbali ya Kivu Kusini ili kujadili masuala ya amani, uchaguzi, na haswa namna gani vijana wanaweza kufikia ngazi za uongozi.

Wakati wa vikao mbalimbali, vijana wamesema wako tayari kushiriki majukumu tofauti kwenye uchaguzi unaopangwa, suala la uchaguzi likiwa mjadala kubwa kwao kabla ya kufikia uongozi. Pia wamechambua baadhi ya changamoto za kisiasa, kiuchumi, kijamii na kiutamaduni, ambazo wamesema mara kwa mara zinawazuia kutimiza malengo yao kisiasa.

Shirika hilo la Karibu Jeunesse Nouvelle kwa ushirikiano na mashirika mengine pamoja na asasi za kiraia, yanazingatia kufuatilia mchakato wa uchaguzi nchini Congo hadi kutangazwa matokeo ya kura zote kwa hali ya utulivu.

XS
SM
MD
LG