Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 11:11

Umoja wa Ulaya wasitisha mpango wa kupeleka waangalizi wa uchaguzi DRC


Rais wa Baraza la Umoja wa Ulaya Charles Michel
Rais wa Baraza la Umoja wa Ulaya Charles Michel

Umoja wa Ulaya umesitisha mpango wa kutuma ujumbe wa waangalizi wa uchaguzi mkuu wa tarehe 20 nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ukisema hautaweza kupeleka watu nchini kote kutokana na sababu za kiusalama.

“Kutokana na changamoto za kiufundi ambazo haziwezi kutatuliwa na Umoja wa Ulaya, tumelazimizika kusitisha kupeleka ujumbe wa waangalizi wa uchaguzi wa EU nchini DRC,” Umoja huo umesema katika taarifa leo Jumatano.

Msemaji wa Umoja wa Ulaya Nabila Massrali aliwambia waandishi wa habari Jumanne kwamba waangalizi wa uchaguzi walikuwa tayari mjini Kinshasa na walitarajiwa kupelekwa nchini kote tarehe 21 Novemba, lakini hawakuweza kwenda kwa sababu za usalama.

Hali ya mvutano inazidi kuongezeka kabla ya uchaguzi wa rais, wa bunge na udiwani katika taifa hilo la pili kubwa barani Afrika, ambalo pia linasumbuka kudhibiti mamia ya makundi yenye silaha katika eneo la mashariki lenye utajiri wa madini.

Kijana mwanaharakati aliuawa jana kwa mawe yaliyorushwa wakati wa kampeni ya mgombea wa upinzani katika mji wa Kindu.

Forum

XS
SM
MD
LG