Kampeni ya uchaguzi ikiwa imefikia wiki yapili Nchini DRC, Mgombea Moise Katumbi amewasili mjini Bukavu kujieleza mbele ya wakazi.
Kumesalia siku 9 pekee kabla ya wapiga kura wa Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo kwenda kuwachagua wabunge wakitaifa, majimbo pamoja na kumchagua raisi mpya.
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo inatazamiwa kufanya uchaguzi wa rais Desemba 20, Sikiliza mpango wa mmoja wa wagombea Mukwege endapo atachaguliwa.
Rais Felix Tshisekedi aliingia madarakani mwaka 2019 baada ya kampeni ya kukosoa rekodi ya haki za binadamu ya mtangulizi wake Joseph Kabila, miongoni mwa mambo mengine. Lakini matukio kadhaa ya hivi karibuni yamezua wasiwasi kuhusu rekodi ya Rais Tshisekedi mwenyewe.
Kiongozi wa upinzani wa Congo anayeishi uhamishoni, Corneille Nangaa siku ya Ijumaa ametangaza kuunda kitengo cha kisiasa cha kijeshi kitakachokuwa mshirika wa kundi la waasi wa M23 na makundi mengine yenye silaha ili “kuiokoa nchi.”
Wiki moja kabla ya raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kupiga kura, Rais Felix Tshisekedi na kiongozi wa upinzani Moise Katumbi na wagombea wengine wameendeleza kampeni zao katika jitihada za kushinda kiti cha juu cha nchi hiyo.
Martin Fayulu si mgeni katika siasa za Congo. Na Pia katika kinyang’anyiro cha urais ameshaonja mikimiki ya kuwania urais katika uchaguzi uliopita ambapo alishika nafasi ya pili.
Kundi la vijana nchini Congo kwa ujumla linaelezewa kuwa linatumika katika harakati mbali mbali za uchaguzi ikiwemo kampeni na masuala mengine ambayo inadaiwa kutumia iwe kwa nia njema au kwa sababu za kuwaridhisha wale ambao wanawatumia.
Wakati Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ikijiandaa kwa uchaguzi wiki ijayo, upinzani na waangalizi huru wanaonya kuwa masuala ikiwa ni pamoja na kadi za wapiga kura zilizofutika, ndege zilizozuiwa katika kampeni, na ucheleweshaji wa orodha ya uchaguzi vinatishia uhalali wa matokeo.
Siku chache kabla mwisho wa kampeni za uchaguzi, bado hali ya ushindani inaendelea Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, DRC, huku kukiwa na mivutano mikubwa kati ya wagombea.
Wagombea kiti cha rais katika uchaguzi wa Disemba 20 nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wanazunguka nchi nzima kunadi siasa na sera zao kukiwepo na idadi kubwa ya wafuasi wanaojitokeza kwa mikutano yao.
Pandisha zaidi