Hali kisiasa na usalama huko Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo imekuwa na wasi wasi mkubwa sana kuelekea uchaguzi wa Desemba 20. Nangaa ambaye ni mkuu wa zamani wa tume ya uchaguzi alitoa tangazo hilo akiwa Nairobi.
Akiwa amesimama pamoja na Bertrand Bisimwa “rais” wa kundi la M23 kwenye hoteli moja katika mji mkuu wa Kenya.
Vitendo vyao vimesababisha zaidi ya watu milioni moja kukimbia nyumba zao, kulingana na Umoja wa Mataifa.
Nangaa ambaye alikuwa rais wa CENI tume ya uchaguzi kwa upigaji kura wa DRC wa mwaka 2018 , hivi sasa anaishi uhamishoni, ametaka kuwepo “muungano wa majeshi yote ya kisiasa, kijamii na kijeshi” katika “kuijenga tena nchi” na “kuirudisha amani” katika taifa hilo maskini liligubikwa na migogoro la Afrika ya Kati.
Amesema kuwa makundi yenye silaha yasiyopungua tisa, likiwemo M23 tayari yameshajiunga na mpango wake "Congo River Alliance" kwa ajili ya “umoja wa kitaifa na utulivu”
Alihalalisha kuundwa kwake kuwa ni majibu kwa “udhaifu” wa serikali ya Congo kwa kipindi cha miongo mitatu na “kushindwa kurudisha mamlaka…katika nchi nzima”
Chanzo cha habari hii ni Shirika la habari la AFP
Forum