Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 03:50

Wapinzani DRC wasema kasoro zinatishia uhalali wa matokeo

 Dkt. Denis Mukwege akipokelewa katika ukumbi wa mji wa Bayonne, kusini-magharibi mwa Ufaransa, Alhamisi Mei 4, 2022. Mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel ya Congo Mukwege alianza kampeni yake ya kuwa rais katika uchaguzi wa mwezi ujao Jumamosi, Novemba 25, 2023, (AP).

Wakati Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ikijiandaa kwa uchaguzi wiki ijayo, upinzani na waangalizi huru wanaonya kuwa masuala ikiwa ni pamoja na kadi za wapiga kura zilizofutika, ndege zilizozuiwa katika kampeni, na ucheleweshaji wa orodha ya uchaguzi vinatishia uhalali wa matokeo.

Kwa miezi kadhaa, tume ya uchaguzi ya CENI imepinga ukosoaji kwa kushindwa kuhakikisha uchaguzi wa huru na haki kama ilivyoahidi, hata ikitaja matatizo ya usafiri na vifaa katika kuandaa kura ya urais na ubunge katika nchi hiyo ya pili kwa ukubwa barani Afrika.

Mivutano imeongezeka katika wiki za mwisho za kampeni kabla ya kura ya Desemba 20. Wapinzani wa Rais Felix Tshisekedi wamelalamikia kile wanachokiita nafasi isiyo sawa ya kushindana na kuibua shutuma ambazo mamlaka zinapanga kuvutia uchaguzi upande wao ikiwa ni pamoja na kutumia daftari la wapiga kura. Hata hivyo tume ya uchaguzi -CENI na ofisi ya rais wanakanusha hili.

Forum

XS
SM
MD
LG