Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 16:50

Tshisekedi, Katumbi na wagombea wengine watoa ahadi kuikomboa DRC


Felix Tshisekedi, kushoto, na Moïse Katumbi.
Felix Tshisekedi, kushoto, na Moïse Katumbi.

Wiki moja kabla ya raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kupiga kura, Rais Felix Tshisekedi na kiongozi wa upinzani Moise Katumbi na wagombea wengine wameendeleza kampeni zao katika jitihada za kushinda kiti cha juu cha nchi hiyo.

Kila upande ukitoa ahadi ya kuikomboa nchi kwa kufufua uchumi na kuendeleza maendeleo ya Taifa. Hubbah Abdi anaangazia Uchumi na Maendeleo ya DRC nchi inapojianda kwa uchanguzi wa Disemba 20.

Ni dakika za lala salama kwa wagombea wa Urais nchini DRC ,ikiwa sasa imesalia wiki moja kabla ya wapiga kura zaidi ya milioni 43 wa Congo kutekeleza haki yao ya kikatiba na kupiga kura tarehe 20 Disemba, Rais wa sasa Félix Tshisekedi akiwania muhula wa pili na wa mwisho wa miaka mitano madarakani huku wagombea wengine akiwemo Moïse Katumbi, mfanyabiashara aliyekuwa gavana wa zamani wa jimbo la Katanga, Martin Fayulu na Dkt. Denis Mukwege ambao wametajwa kuwa wapinzani wakuu.

Martin Fayulu, kushoto na Denis Mukwege. Picha na (Photo by AFP)
Martin Fayulu, kushoto na Denis Mukwege. Picha na (Photo by AFP)

Lakini tuangalie uchumi wa DRC…. Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ni nchi kubwa zaidi ya Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara. Wadadisi wa masuala ya kiuchumi wakiulinganisha na Ukubwa unaokaribia bara ulaya lenye idadi ya watu wanaokadiriwa kuwa zaidi ya milioni 100, nchi hiyo ina utajiri mkubwa wa maliasili.

Hata hivyo licha ya ukwasi wa taifa hilo Raia wanahisi kukabiliana na ugumu wa maisha huku maswali kuhusu athari zinazoweza kujitokeza katika maendeleo ya uchumi wa taifa na mwelekeo wake wa siku zijazo. Hubert Masomeko ni mtaalam wa Siasa na Uchumi nchini DRC

Hubert Masomeko -Mtaalam wa Siasa na Uchumi-DRC anaeleza: DRC inaweza isiwe nchi iliyoendelea zaidi katika eneo la Maziwa Makuu, lakini rasilimali zake kubwa na tofauti za madini zinaonyesha uwezekano mkubwa wa maendeleo. Nchi ni muuzaji mkuubwa wa madini ya cobalti, shaba, almasi, coltan na bati kwa masoko ya kimataifa.

Ingawa madini kama shaba, almasi na bati yanajulikana vyema kwa umma, huenda isiwe hivyo kwa madini ya kobalti na koltani. Hata hivyo mzozo juu ya upatikanaji wa rasilimali hizi muhimu imekuwa moja ya sababu za kukosekana kwa amani kwa muda mrefu na na kuiweka DRC katika taswira ya machafuko miaka nenda miaka rudi.

Itakumbukwa Mnamo 2019, Rais Felix Tshisekedi aliahidi kuifanya DRC kuwa kama taifa la Ujerumani barani Afrika na kuahidi kujenga kiwanda cha betri kwa kutumia madini yanayochimbwa nchini DRC, Lakini ahadi ambayo ingeikwamua DRC kutoka kwa lindi la umaskini kwa asilimia fulani bado halijafanikiwa katika nchi iliyo na upungufu wa umeme mara kwa mara na utaalam mdogo wa utengenezaji. Kwa raia wengi, ukuaji wa uchumi upo kwenye karatasi kwa sasa.

Wafuasi wa Rais Felix Tshisekedi wakisubiri kuwasili kwake katika kampeni huko Goma, Mashariki ya Congo, Jumapili, Dec. 10, 2023. Tshisekedi anawania tena nafasi ya urais katika uchaguzi wa Desemba 20. (AP Photo/Moses Sawasawa).
Wafuasi wa Rais Felix Tshisekedi wakisubiri kuwasili kwake katika kampeni huko Goma, Mashariki ya Congo, Jumapili, Dec. 10, 2023. Tshisekedi anawania tena nafasi ya urais katika uchaguzi wa Desemba 20. (AP Photo/Moses Sawasawa).

Ingawa utajiri wake mkubwa wa madini na idadi kubwa ya watu inawakilisha rasilimali kubwa ya kiuchumi, maisha nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo hayajaboreka kwa watu wengi kwa sababu kadhaa, kama vile migogoro, rushwa na miongo mingi ya utawala mbovu tangu enzi za ukoloni.

Huku kampeini zikishika kasi …kila anayewania akiahidi kuboresha uchumi na kuimarisha maendelo ya DRC hata hivyo mchambuzi Oscar Moshi - Mtaalam wa sera - DRC anasema wakati wa kampeini viongozi wengi wanawahadaa wapiga kura kwa ahadi tele lakini bila kutimiza azma na malengo ya ilani zao za vyama.

Kauli ya Oscar ikiungwa mkono na Hubert anayekiri kuwa wote wanaowania uongozi walikuwa na bado wako serikalini lakini uchumi wa DRC imezidi kuwa mbaya.

Hubert Masomeko -Mtaalam wa Siasa na Uchumi-DRC anasema: "Hata hivyo tangu Rais Felix Tshisekedi aliposhinda katika uchaguzi wa 2019 Tshisekedi amefanikisha baadhi ya mafanikio katika sekta ya uchumi. Na japo Kiwango cha ukuaji wa Pato la Taifa kilipungua wakati wa janga la Covid 19 Iliongezeka hadi asilimia 8.92 mwaka 2022 kutoka asilimia 6.20 mwaka 2021, huku sekta ya madini ikichangia zaidi."

Chini ya utawala wa Tshikedi mnamo 2022, DRC ilijiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki kama mwanachama wake wa saba. Matumaini ya Tshisekedi yalikuwa kwamba hatua hii ingekuza uhusiano wa kibiashara na kupunguza mivutano na majirani wa DRC. Kuingia katika jumuiya kunaipatia DRC fursa ya kupata soko la watumiaji milioni 146 na inamaanisha inaweza kuanza kuagiza bidhaa zaidi kutoka kwa majirani zake wa Afrika mashariki.

Hata hivyo, msukumo kutoka kwa wagombea wa upinzani wanaokosoa mafanikio ya serikali ya Tshisekedi inamaanisha atahitaji kufanya kampeni kwa bidii ili kushinda.

Katika siku chache Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo inatazamiwa kufanya uchaguzi muhimu ambao unavutia hisia za kimataifa. Uchaguzi huu ujao, uliopangwa kufanyika Desemba una umuhimu mkubwa sio tu kwa DRC bali bara zima la Afrika.

Imetayarishwa na mwandishi wetu Hubbah Abdi, Washington, DC.

Forum

XS
SM
MD
LG