Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 17:07

DRC yaiomba msaada UN katika usambazaji wa vifaa vya uchaguzi


Ujumbe wa kulinda amani ukiwa katika misheni ya Umoja wa Mataifa huko DRC (MONUSCO) Decemba 20, 2016. Picha na REUTERS/Thomas Mukoya
Ujumbe wa kulinda amani ukiwa katika misheni ya Umoja wa Mataifa huko DRC (MONUSCO) Decemba 20, 2016. Picha na REUTERS/Thomas Mukoya

Serikali ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo imeiomba Umoja wa Mataifa kuruhusu kikosi cha kulinda amani kusaidia katika usambazaji wa vifaa kwa ajili ya uchaguzi mkuu utakaofanyika wiki ijayo, kwa mujibu wa barua iliyoonekana na Shirika la habari la Reuters.

Kumekuwepo na changamoto katika usambazaji wa vifaa vya kupigia kura katika nchi hiyo ya pili kwa ukubwa barani Afrika, kutoakana na kutokuwa na barabaza za lami pamoja na migogoro ya waasi katika majimbo ya Mashariki mwa nchi, ambako kikosi cha Umoja wa Mataifa cha kulinda amani kimepelekwa.

Ujumbe unaojulikana kama MONUSCO, tayari umeanza kusambaza vifaa vya kupigia kura katika majimbo ya Ituri, Kivu Kaskazini na Kivu Kusini. Mamlaka yake kwa sasa yako katika maeneo hayo tu.

Wakati huo huo, mmoja wa wagombea wakuu wa upinzani katika uchaguzi mkuu wa urais wa Jamahuri ya Kidemokrasi ya Congoutakaofanyika wiki ijayo, Moise Katumbi ameahirisha sehemu ya kampeni zake leo baada ya ghasia kutokea katika moja ya mikutano yake ya kampeni.

Risasi zilifyatuliwa na baadhi ya watu walijeruhiwa wakati Katumbi akihutubia wafuasi wake katika mji wa Moanda siku ya Jumanne na kuashiria kuongezeka mvutano kabla ya uchaguzi mkuu Decemba 20.

Kumekuwa na matukio tofauti, serikali ya jimbo ilisema katika taarifa yake kwamba walinzi wa Katumbi walifyatua risasi za onyo baada ya kundi la watu kuongeza fujo na kuzua hali ya wasiwasi na mivutano. Polisi walitumia mabomu ya machozi kurejesha hali ya utulivu.

Watu kadhaa walijeruhiwa akiwepo afisa wa polisi ambaye aliumizwa vibaya na uchunguzi kufuatia tukio hilo unaendelea, taarifa hiyo imeeleza zaidi.

Katumbi alisema katika mtandao wa X ambao awali ulijulikana kama Twitter kwamba polisi walifyatua risasi dhidi ya watu na tukio hilo limetengenezwa kuchochea ghasia.

Forum

XS
SM
MD
LG