Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 17:08

DRC inaanza kampeni ya uchaguzi wa rais na wabunge Jumatatu


Mkutano wa kampeni DRC kwa wafuasi wa Martin Fayulu Novemba 21, 2018. Reuters.
Mkutano wa kampeni DRC kwa wafuasi wa Martin Fayulu Novemba 21, 2018. Reuters.

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo inaanza kampeni ya uchaguzi wa rais ya mwezi mmoja siku ya Jumatatu huku wagombea 26 wakiwania urais huku kukiwa na hali ya wasiwasi ya kisiasa na mapigano mashariki mwa nchi hiyo

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo inaanza kampeni ya uchaguzi ya mwezi mmoja siku ya Jumatatu huku wagombea 26 wakiwania urais huku kukiwa na hali ya wasiwasi ya kisiasa na mapigano mashariki mwa nchi hiyo

Takriban wapiga kura milioni 44 waliojiandikisha, kati ya wakazi karibu milioni 100, watamchagua rais Desemba 20.

Pia watachagua kati ya maelfu ya wagombea ubunge na wajumbe wa serikali za mitaa katika nchi yenye rasilimali nyingi lakini imegubikwa na migogoro na ufisadi.

Kampeni ya mapema imekuwa ikiendelea kwa muda, huku Rais Felix Tshisekedi, ambaye anawania muhula wa pili, akihudhuria hafla nyingi za umma huku washirika wake wakisifia rekodi yake.

Forum

XS
SM
MD
LG